Pongezi Rais Magufuli kwa kujali wajawazito

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MARA nyingi tumekuwa tukisikia taarifa katika vyombo vya habari au hata kuona wenyewe wajawazito wengi katika hospitali kubwa wakiwa wamelala chini au kulala zaidi ya mtu mmoja katika kitanda kimoja. Kila mmoja anafahamu ukubwa wa vitanda vya hospitalini, hivyo kulala mtu zaidi ya mmoja inakuwa vigumu kiasi tena ukizingatia mtu yuko katika ujauzito.

Wanawake wanafahamu hali inavyokuwa kwa mjamzito, hivyo kulala chini au kulala kitanda kimoja wawili au watatu, hakika unapata kero kubwa jambo linalopaswa kuangaliwa kwa jicho la tofauti.

Mapema mwezi huu, Rais John Magufuli alitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumuangalia Mufti Mkuu wa Tanzania, Shekhe Abubakar Zubeiry, aliyekuwa amelazwa hospitalini hapo na alipokuwa akitoka katika wadi ya Mufti, wanawake hospitalini hapo walimuomba kuona jinsi wanavyopata tabu.

Baada ya kuingia wadini hapo alifadhaika jinsi wajawazito walivyokuwa wamelala kitanda kimoja zaidi ya watano na baada ya kuondoka, alichukua uamuzi wa kubadili jengo moja la ofisi kuwa wadi ya akinamama na kusaidia waliolala chini kupata vitanda.

Hakika uamuzi huo ulikuwa kweli wa kiongozi na umetatua tatizo hilo mara moja hivyo ni vyema sehemu nyingine kama hospitali za wilaya na mikoa, viongozi wahakikishe wanakuwa na uamuzi wa busara wa ukombozi wa mwanamke.

Hakika kwa hili alilofanya Rais katika kuwasaidia waliokuwa wakipata matibabu, amesaidia wanawake wengi nchini ambao kwa sasa wanajisikia furaha wakijua wakienda Muhimbili, hakuna tatizo la vitanda.

Ni vyema viongozi wengine nchi nzima walione hilo na kuiga mfano ili kumkomboa mwanamke kwa kuchukua uamuzi utakaomsaidia mwanamke hasa akiwa mjamzito ili kumpunguzia changamoto za wakati huo.

Hongera sana Rais Magufuli katika hili hakika umeonesha nia yako ya kumkomboa mwanamke wa Tanzania katika kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuanzia na hili la afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…