Pongezi kwa waliopaza sauti kupitia JF kuhusu anajiita "Kiboko ya Wachawi"

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
1,033
895
Natoa pongezi kwa wale waliokuwa wanakwazika na habari zilizokuwa zinarushwa hewani kupitia redio kuanzia saa 6 usiku hadi saa 11 alfajiri.

Kupitia hapahapa JF kulikuwa na maandiko kadhaa kuelekea TCRA kuwa wajiridhishe kuhusu kituo cha Redio kinachorusha habari zake, takribani wiki sasa redio iliyokuwa inarusha matangazo yanayomhusu anajiita "Kiboko ya Wachawi" haisikiki.

Kama habari hizo za kituo cha Redio kutokuwa hewani zinahusiana na kuruhusu kurusha matangazo ya anayejiita "Kiboko ya Wachawi" ni za kweli TCRA itoe tamko ili iwe fundisho kwa vituo vya Redio vingine.

Pia Soma: DOKEZO - Serikali chukueni hatua za haraka dhidi ya Nabii Dominiki "Kiboko ya Wachawi"
 
Redio gani hiyo, ni hizi fm za mitaani? Hata wale wanaojiita mitume na manabii, makuhani, madokta wakati matendo na maisha yao hayaakisi huduma hizo ni wa kutupiwa jicho pevu.
Hakika mkuu,
Huku kwetu ( Mpanda Katavi) pia kuna manabii wa Kariba hii na hutumia Fm Radio za Kijamii kuwahadaa na kuwatapeli wananchi. Tcra tumeni watu wenu kimyakimya huku hii Radio iliyoko mopandahotel siiamini kabisa.
 
Ila kule Iringa uchawi ulizuia umeme wa Tanesco usipite ujue!😯


Ipo siku ntaelezea hii science Ila ukiona unagusika na haya mambo ujue una tatizo .

Mchawi huwa anaendeshwa Ila yeye haendeshi .

Watu wengi wanasumbuliwa na maswala ya AKILI Psychological disorder , Ila wanadhani wamerogwa.

Wachunganji na baadhi ya mashekh hutumia Uchawi Kama njia ya kujipatia kipato .

Ukiwa innocence , unakuwa haugusiki Ila ndo hivyo watu hawana haya maarifa ya gizani wameishia kuamini uchawi.
 
Yako matapeli mengine yamejaa tele mitandaoni yakitumia dini kutapeli, tena yameenda mbali kwa kujifanya ni wachekeshaji yakiwaambia watu hayajawahi kufika mbinguni yenyewe yatafundisha uhalisia, habari za mbinguni wamewaachia wachungaji wafundishe
 
Vipo vituo vingine vinarusha matangazo ya aina hiyo hata ya waganga wa kienyeji na shuhuda zao feki. Tunalipotosha taifa na kurudisha nyuma maendeleo kwa kuendekeza huu upumbavu kwa kisingizio cha uhuru wa imani.
 
Mkuu
Ni vile mpiga mbiu aliweka hoja makini sana kuhusu shughuli za huyo nabii, lakini tusijisahau kuwa hakuna kitu ambacho kinafanyika bila serikali kufahamu.

Nashawishika kuamini kwamba serikali ina jambo lake kwenye hili na sisi raia tumestuka mapema ndo maana wanajifanya kuchukua hatua kimya kimya....
 
Vituo vya redio vinavyorusha huu upuuzi serikali ivimulike na kuvifunga. Tunajenga taifa la mataahira kwa uchu wa pesa wa matapeli. Wenzetu wanadanya mambo ya maana sisi tunabaki mpaka kuagiza toothpick na yeboyebo wakati malighafi za kutengeneza vitu hivyo tunazo. Kazi yetu kwenda usiku kucha kumpayukia mungu kiziwi sala na maombi ya abracadabra! Hatujifunzi hata kwa binadamu ambaye Mungu meenyewe amesema sisi ni SURA NA MFANO WAKE. Wewe upo chumbani mtoto wako usiku kucha yupo hapo mlangoni anakupigia kelele usiku kucha anaomba nauli ya kwenda shule!! Huko ndiko huu ulokole ulipofikia. I dare to say hawa si wakristo. Ni kichekesho tu hata imessbabisha watu wa imani zingine kuudharau ukristo.
 
Yeah,uko sahihi. Ukipandisha spiritual vibration Energy to a certain level kwa kufanya meditation ama yoga. Mchawi hawezi kukufikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…