Pongezi kwa Madaktari wetu bingwa katika hospitali ya Muhimbili Mloganzila kwa kupandikiza uliyo kwa wagonjwa

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,606
8,406
Kwa mara nyingine tena Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili Mloganzila imefanikiwa kupandikiza uloto kwa wagonjwa mbalimbali walio fikishwa hapo, jambo hilo ni hatua kubwa kwa taaluma ya udaktari lakini pia inaokoa gharama kubwa ambazo zingetumika kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Tunaiomba serikali iendelee kuwekeza vifaa tiba vingi zaidi katika Hospotali yetu ya Taifa ya Mloganzila kwani hadi sasa ndio hospitali inayo tegemewa kitaifa na Kimataifa.

Pia nashauri uwanja wa ndege ujengwe kwenye eneo hilo.

Eneo ilipo Hospitali ya Taifa Mloganzila ndipo haswa panafaa kuwa hospitali kwani ni patulivu na pana nafasi ya kutosha, wagonjwa na hata madaktari na wauguzi hawana stress.
 
Duh imebidi nigugo maana uloto, kumbe ni bone marrow? Na uboho ni nini?
 
Back
Top Bottom