Polisi wazingira mgodi wa Bulyanhulu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,124
Thursday, May 25, 2017
Polisi wazingira mgodi wa Bulyanhulu





Kwa ufupi
  • Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anayetoka wala kuingia.
By Peter Saramba, Mwananchi
Kahama. Jeshi la Polisi limeuzingira mgodi wa Bulyanhulu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia katika mgodi huo alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).

Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Mapema leo, Mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.

Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.
 
I am result oriented person... Yes, it sounds good and I like it lakini muhimu kwangu score board itasoma nini baada ya dakika 90!!

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!! Unaweza kuta tunashangalia vyenga, makanzu, matobo na kila mbwembwe za soka! Tunashambulia lango la adui kama nyuki!

In no time, inapigwa bonge la counterattack na sekunde 10 baadae, tunaokota mpira kwenye nyavu zetu wenyewe!!!

Haidhuru, wapo watakaokuja na kusema... sio kwa Stars hii ya Samatta!
 
Inahitajika busara kubwa sana kuihandle hii ishu, bila shaka wanasheria wa ACACIA wapo chimbo wanajipanga, natamani na wa kwetu wawe maeneo wakiandaa nondo za kutetea kilicho chetu........vinginevyo tutakuja kutupiana Mpira hapa, kila MTU akikana msimamo wake na mwisho ikawa aibu kwa TAIFA.
 
Wale vigogo wa mgodi waliokaidi amri ya mkuu wa mkoa watiwe ndani for 48 hours ili washike adabu, ila hawa wengine 'manamba' waachiwe waenende zao kwa 'Amani ya Bwana'. Wao sio decision maker kwa hiyo hawakuwa na maamuzi ya nani aingine na nani asiingie mgodini... Pole mkuu wa mkoa kwa kudharauliwa ndani ya himaya yako!
 
Tuliokuwepo 67 tunakumbuka maandamano na majina tuliyowaita watu. Ubepari ni unyama, ni kama wanyama wa mwituni........! Yaliishia wapi? Hata kabla mwalimu hajaaga tulishageuka mawe aliyokataa kugeuka. Nini maana ya utandawazi. Mchina alianza na ukomunisti wake sasa hivi anawazidi hata mabepari waliomtangulia. Kuna wachina wana pesa kuliko serikali yoyote ya Afrika. Waulize wacuba, Venezuela na aina yao kiko wapi?
 

Ndiyo maana Lissu alisema tujitoe kwanza MIGA mengineyo tutayafanya taratibu. Ameuona Mkataba wa Bulynkulu anajua vyema ulivyo na madudu na shareholders wengine ni wale tuliowapa Dhamana ya kuongoza.

Siyo Mara ya kwanza Migodi kuwakatalia Viongozi kuingia ndani,walimkatalaia waziri na ujumbe wake tena waziri mwenye dhamana sembuse mkuu wa Mkoa anayejua KKK.

Tukiambiwa mikataba ni mbovu ndiyo sababu wanafanya hivi kwa taratibu wanajua wapi watatushika tu.

Kumbukeni kuna akina Mkapa na JK huko msije mkasema hatukuambiwa.

Tuwasikilize na mawazo ya wengine tupate kushinda kama tunafikiri tu kumsikiliza Mpinzani atapata kick basi tumeumia.

Kama.Lissu alishaipata alipowatetea wale 328 waliozikwa kwenye KABURI moja tena bila kulipa senti tano

Na serikali yenu mwaka juzi imefanya mazishi yao pamoja na Mkapa kukataa kwamba kulikuwa hakuna Watanzania, ndiyo sababu akasema dhahabu ni bora kuliko Mtanzania wengine hawakumuelewa
 

Pole sana Majangili wala siyo wazungu ni Watanzania wenzetu tuliowapa Dhamana akina Che Mkapa na JK.Usiwalaumu wazungu wakati kuna Watanzania wanaakili za kujaza choo tu.Wanafikiria matumbo yao ndiyo sababu sitompongeza wala kumpigia makofi Magufuli maana alikuwepo kwenye kufunga sheria zenye ukakasi,wakawatukana Wapinzani tena kwa mbwembwe za kuwaita kila majina mabaya leo ati tuwaite wazalendo kwa lipi.

Mafuta Majanga hula na wakwao
 
Umenisoma na kunielewa lakini? Mawazo yangu na ya kwako ni sawa tumetofautiana presentation. Mimi nimetoka nyuma zaidi yako. Rudia kusoma nilichoandika.
 
Mkuu wa mkoa sifa yake ni kusoma na kuandika tu, sasa huyo mama anawezaje ku challenge geologists wakati yeye KK mbili tu ndio uwezo wake na ile K ya kuhesabu haina maana kwake. Jibu ni kuwa ameenda pale kutafuta KIKI. Hizi kiki zitatuponza, wakati huu kamati ya wanasheria na wataalam wa uchumi inamalizia kazi ilitakiwa watanzania tuwe watulivu akiwemo mkuu wa mkoa. Sijaona mahali Mh Raisi amewaambia wasimamishe uzalishaji, na TMAA imetumbuliwa uongozi nashangaa wizara imeshindwa kuoganaizi haraka kazi ziendelee kwa mujibu wa mkataba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…