View attachment 353806
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasilisha Mkataba wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za kuishi askari eneo la Kunduchi, Mikocheni pamoja na Kituo cha polisi cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam, mradi unaohusisha pia majengo mbalimbali ya Mwekezaji ambaye Jeshi la Polisi limeingia nae Mkataba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Jenerali Rwegasira amesema mradi huo ni mkubwa sana na wa muda mrefu na hivyo ameliagiza jeshi hilo kuuwasilisha Mkataba huo ambao utekelezaji wake unaendelea ili aweze kuufahamu vizuri mkataba huo unaolihusisha Jeshi la Polisi na Mwekezaji wa Kampuni ya Mara World Tanzania limited.
Jenerali Rwegasira ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki muda mfupi baada ya kukagua miradi hiyo katika maeneo ya Kunduchi na Mikocheni ambako zinajengwa nyumba za kuishi askari wa jeshi la Polisi na kwamba ujenzi wake bado unaendelea.
Jenerali Rwegasira ametembelea pia mradi wa ujenzi wa Kituo cha Polisi eneo la Polisi Oysterbay ili kuona maendeleo ya ujenzi huo sambamba na kufahamu hatua iliyofikiwa hadi sasa katika maeneo hayo ya jeshi la polisi.
Aidha mwekezaji huyo ambaye ni Kampuni ya Mara World Tanzania limited katika eneo la Polisi Oysterbay atajenga kituo cha polisi cha kisasa, ofisi za kukodisha, hospitali, maduka makubwa na hoteli.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
5 Juni, 2016.
My Take:
Sasa Kimenuka rasmi.