Polisi wana mamlaka ya kuamrisha mtu kupimwa??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,121
Nimeuliza zaid ya mara moja . Lakn sijapata msaada wa kisheria. Nauliza tena . Police wana mamlaka ya kumpima mtu kwa mkemia mkuu bila kupitia kokote?? Chombo cha juu kabisa kutoa agizo ni na ulazima wa kutekelezwa ni mahakama. Police wanapata wapi mamlaka kwenda kumpima mtu kwa mkemia mkuu wa serikali ndipo baadaye wampeleke mahakamani.

Kama hivyo ndivyo kwanini isiwe lazma kumpima mtu mwenye ukimwi. Mwenye matatizo ya akili wapo wengi sana na wanaleta madhara. Lakn amri ya kuwapima akili zao hutolewa na mahakama tu.
Hii ya madawa ya kulevya kwamba kila anayekamatwa anaenda kupinwa kwa amri toka kwa nani hapo police? Na je nikikataa napewa adhabu gani??

Nimepitia katika sheria ya madawa ya kulevya sijaona sehem ya watu kwenda kupimwa kwa mkemia kwa amri ya police. Kama sijasoma vizuri niko tayar kukosolewa au niseme kuelekezwa. Binafs naona police wanawadhalilisha wanaenda kuwapima bila kufuata taratibu husika. Sheria mpya ya madawa ya kulevya hii hapa chini

http://www.lrct.go.tz/download/translated-laws/kiswahili-vision/SHERIA YA MADAWA YA KULEVYA.pdf
 
Polisi haijui mipaka yake!Hata kuhojiwa ni hiari ya mtu,mtu anaweza akaamua kutotoa ushirikiano anapokamatwa na polisi!Ni hiari ya mtu pia kupimwa,sasa hili limegeuzwa sharti!
 
Napendekeza serikali iwapime watanzania wote na kila atakayekutwa aliwahi kutumia ashitakiwe mahakamani
 
Asante mkuu kwa kulianzisha hili, ila ukweli nchi inaendeshwa kidikteta. Uzuri ni kwamba haya mamlaka yanaishia hapa hapa duniani. Kifo kipo kwa kila nafsi hata Dikteta ataulaza na maiti yake itazomewa
 
Napendekeza serikali iwapime watanzania wote na kila atakayekutwa aliwahi kutumia ashitakiwe mahakamani
Hahahah. Hii itakuwa hatari maana hata mtanzania namba wani kwa anavyokurupuka ni wazi kabisa inaweza kuwa athari za ngada au weed au tertiary sphyllis
 
Polisi siyo kazi yao kuamrisha watu wapimwe kama wanatumia madawa ya kulevya. Hiyo ni kazi ya mahakama baada ya kuombwa na Polisi.
Vinginevyo Polisi ingekamata watu na kuwapeleka wakapimwe Kichaa au kifafa kabla ya kesi..
Hapa kutakuwa na mchezo wa kutaka kuchafua mtu mbele ya jamii tu.. Ndiyo maana hata wito wa maandishi hawataki kutoa bali wanataka baadaye wakane kuita mtu nje ya taratibu..
 
Ngoja zamu yako ifike ndio utapata majibu sahihi kwa hili swali lako mkuu.
Kuna mtu alienda na mawakili 200 lakini mwisho wa siku alipimwa na kilichojiri ni public info.
 
Ulitakiwa kujiuliza kabla Police wamepewa mamlaka kupeleleza kesi?Anzia hapo.Tofauti ya mahakama kuruhusu mtu kupimwa ni issue inaporise either ktk defence au vyovyote vile inayohitaji ushahidi wa kitaalamu ndipo mahakama hutoa amri ushahidi utafutwe kwa njia ya kitaalam na si vinginevyo.Vinginevyo utaendelea kuuliza .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…