Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemtia mbaroni Mtu mmoja aitwaye Emmanuel Sulwa Mapana (24) maarufu Mchambi Mkazi wa Mtaa wa Sima, Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania zenye cheo cha Luteni.
Polisi Simiyu wamesema leo February 14,2025 saa 6:30 mchana Kikosi kazi cha kupambana na uhalifu na Wahalifu Mkoa wa Simiyu kilifanikiwa kumkamata Mtu huyo akiwa amevaa Kombati ya Jeshi la Wananchi Tanzania akiwa na gari aina ya Ractic lenye namba ya usajili T.560 DCS ambapo pia alikutwa na Mkanda wa Jeshi la Wananchi na Laptop 01.
“Emmanuel Sulwa Mapana alikuwa anatafutwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa kosa la kujifanya Mtumishi wa Serikali, Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa Wananchi wote kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za uhalifu na Wahalifu” - imeeleza taarifa ya Polisi. #MillardAyoUPDATES