Polisi wamezingira nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Joseph Gwajima

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
56,667
30,584
Tutaendelea kuwapa yanayojiri.

Mchezo huu hautaki hasira

=> Polisi 6 ndani ya Landcruiser wako nje ya nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wamezingira nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Joseph Gwajima huko Salasala, jijini Dar muda huu.

Wasema wamegonga geti bila kufunguliwa.


=======

Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo linamuhitaji Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa kuwa kuna mkanda wameupata unaosemekana ni wake ambao unazungumza maneno ya kichochezi.

Kamanda Sirro alisema: “Tumepata clip (mkanda) inayosemekama ni ya kwake. Tunamtaka athibitishe kama hayo maneno ni ya kwake. Na kama ni yeye ameyasema, anaelewa nini kuhusu kile alichokizungumza kwa sababu hayo maneno ni kichochezi. Tupo kwenye uchunguzi mama yangu.”

Jana, polisi jana walipiga kambi kwa saa saba kwenye geti la nyumba ya Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wakitaka kumkamata bila ya mafanikio.

Polisi hao walikuwa kama wageni wa askofu huyo wakisubiri wafunguliwe geti, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:10 jioni walipoamua kuondoka wakitumia gari aina ya Toyota Landcruser lenye namba za kiraia, ambalo kwa muda wote huo lilikuwa limeegeshwa pembeni mwa geti hilo.

Chanzo: Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…