Polisi toeni elimu kwa raia suala la kulawitiwa binti wa Yombo

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,502
9,488
Habari.
Leo ni siku ya tatu toka toka nipate taarifa juu ya sakata la msichana ambaye kimuonekano hata miaka 20 bado hajafikisha mkazi wa Yombo Dovya.

Nikiwa kama raia na mtumiaji mkubwa wa mitandao nimebahatika kuona habari zake kupitia maandishi na picha kwani mpaka sasa sijabahatika kuiona hiyo video yq ukatili huo na sitohitaji kuiona nikiwa kama mzazi wa watoto wa kike.

"Inasemekana" nanukuu waliofanya tukio hilo ni wanajeshi ambao walikuwa wamefata maagizo ya afande wao ambae katika hyo video hakutajwa jina lakini moja ya sababu kubwa ni binti huyo kushiriki/kuwa na mahusiano na mme wa afande huyo.

Picha zilipigwa na video zilichukuliwa zikionyesha watuhumiwa wakimfanyia kitendo cha ulawiti binti huyo kwa kumuingilia kwa zamu kisha video hizo kusambazwa katika mitandao ya kijamii.

MATOKEO YA TUKIO HILO.
Tukio hilo limeibua gumzo ndani ya nchi na mitandaoni kwa ujumla kwani taasisi mbali mbali pamoja na wananchi kwa ujumla wameomba hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa wa tukio hilo.

Tukio limeenda mbali zaidi kwa watuhumiwa kuhusishwa na jeshi letu, kwa kutumwa baadhi ya picha za watuhumiwa wakiwa wamevaa sare za jeshi letu ambalo naweza kusema ndio chombo kikubwa cha ulinzi ambacho asilimia kubwa ya wananchi tuna imani nacho.

Hivyo basi.
Nikiwa na imani kubwa na jeshi langu la Tanzania na mapenzi makubwa na nchi yangu naomba jeshi letu tukufu litoe taarifa rasmi kuhusiana na tuhuma hizi na hatua walizochukua au watazochukua
a) Endapo watuhumiwa ni watumishi/walikuwa watumishi wa jeshi

b)Endapo watuhumiwa si watumishi wa jeshi letu ikiambatana na onyo kali kwa wote wataobainika kulihusisha tukio hili na jeshi letu la wananchi.

Kwa jeshi langu la polisi.
Endapo tukio hili lilifanywa na askari wa jeshi la wananchi tunaomba jeshi letu la polisi mtoe elimu kwa raia jinsi ya kudeal na watuhumiwa waliofanya uhalifu ambao ni watumishi wa jeshi huwa kuna procedure zipi za kuchukua.

Kwani nijuavyo mimi mchakato wa kumkamata mwanajeshi aliyefanya kosa kama lilivyofanywa kwa huyu binti huanzia jeshini.

Kwa watuhumiwa kukamatwa na military police(m.p) baada ya ushahidi kuwa sawa na watuhumiwa kushikwa na hatia hufukuzwa kazi kupitia court martial (mahakama ya kijeshi) endapo walifanya kosa nje ya jeshi, kisha kukabidhiwa kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kumalizia uchunguzi na kufikishwa mahakama ya kiraia wakiwa si wanajeshi.

Kukosekana kwa elimu tajwa hapo juu imeendelea kuleta sintofahamu ndani ya jamii na kuibuka taarifa nyingi za uongo nyingi zikidhalilisha na kuvidharaulisha vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndani na nje ya nchi kwani yanayoandikwa hayaishii ndani tu bali yanafikia dunia nzima.

Kuepusha mpanganyiko huu na sintofahamu ningeshauri serikali yangu sikivu ikipendeza izichukue hatu tajwa hapo juu ili kuendelea kuitunza amani na upendo ikiwa na mshikamano kama taifa.

Ahsanteni

PIA SOMA
- Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu
 
Amini nakuambia kama waliofanya hilo tukio ni wanajeshi hakuna chechote watafanywa zaidi ya blahblah tu
 
Amini nakuambia kama waliofanya hilo tukio ni wanajeshi hakuna chechote watafanywa zaidi ya blahblah tu
Issue kwa sasa ni tete watu wengi maskio yako wazi na midomo pia hakuna aliye juu ya sheria mkuu sema kuna hatua zinafanyiwa kazi ambazo wengi hatutajua how
 
Issue kwa sasa ni tete watu wengi maskio yako wazi na midomo pia hakuna aliye juu ya sheria mkuu sema kuna hatua zinafanyiwa kazi ambazo wengi hatutajua how
Hatua ipi tena wakati kila kitu kipo wazi? Laiti angechoma picha ya samia saivi unadhani angekuwa wapi huyo mtu?
 
Back
Top Bottom