JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,628
- 6,294
Akiongea katika eneo ambalo wananchi walitoa kilio chao juu ya ajali za mara kwa mara Mkuu wa kikosi cha usalama Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa wapo kaika ukaguzi na kuangalia maeneo yenye changamoto ikiwa ni Pamoja na eneo hilo la kisongo wilaya ya Arumeru ambalo wananchi walitoa kilio chao juu ya uwekaji wa vidhibiti mwendo.
Aidha ametoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa Barabara kuhakikisha wanafuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali ambazo zinasababishwa na kutokufuata sheria zilizopo.
Mhandisi Newton Matemba kutoka ofisi ya wakala ya Barabara Tanroads Mkoa wa Arusha ambaye anashughulika na kitengo cha Usalama Barabarani yeye akabainisha kuwa wamepokea kilio cha wananchi wa eneo hilo na maeneo mengine huku akiweka wazi kuwa maeneo yote yanafanyiwa tathimini na kuweka alama za barabarani ili kukomesha ajali ambazo zimekuwa zikitokea.
Nae mwenyekiti wa kitongoji cha Ematasha Kisongo wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha licha ya kuzishukuru mamlaka hizo kufika eneo hilo amesema kuwa eneo hilo zimekuwa zikitokea ajali eneo hilo kutokana na madereva Kwenda mwendo kasi eneo hilo akiomba vidhibiti mwendo kuwekwa kwa wakati kudhibiti changamoto hiyo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Arusha