Polisi: Mzee Philip Mangula amekutwa na sumu mwilini, ni baada ya kufanyiwa uchunguzi

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,242
4,645
Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ikishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na Taasisi mbalimbali imebaini kwamba ndani ya mwili wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mzee Mangula kulipatikana na sumu,uchunguzi kuhusu tuhuma ya sumu hiyo ilivyoingia mwilini upelelezi bado unaendelea.

Ikumbukwe wiki iliyopita, Mzee Mangula akiwa kwenye majukumu yake alianguka ghafla na kukimbizwa hospitali ambapo alilazwa kwenye chumba cha uangalizi maalum (ICU)

Pia soma > Dar: Philip Mangula aanguka gafla, alazwa ICU. Rais Magufuli amjulia hali

Mangula.jpg


TAARIFA KWA UMMA.

UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA KUWEKEWA SUMU NDG.PHILIP MANGULA

Mnamo tarehe 02/03/2020 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipokea taarifa kutoka kwa uongozi wa chama cha mapinduzi ya kuwekewa sumu makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula,

Mnamo tarehe 28/02/2020 Mzee Mangula alidondoka ghafla katika makao makuu ndogo ya CCM Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha kamati kuu ya Almashauri kuu ya CCM iliyokuwa ikijadiri mambo mbalimbali ya chama likwemo suala la adhabu ya wanachama watatu ambao walikuwa na tuhuma mbalimbali za ukiukwaji wa maadili ndani ya chama hicho.

Katika taarifa hiyo tulielezwa kwamba Mzee MANGULA alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili amabapo alilazwa katika chumba cha uangalizi wa karibu (ICU).

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam likishirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na taasisi mbalimbali limebaini kwambandani ya mwili wa Mzee Mangula kulikuwa na sumu.Uchunguzi kuhusu namna sumu hiyo ilivyoingia mwili mwake bado unaendelea kufanyika.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam litachukua hatua kali kwa mtu yeyote atakaye bainika kupanga ,kuratibu na kutekeleza uhalifu huo awe ni mwana familia ,kutoka ndani ya chama ,nje ya chama ,ndani ya nchi au nje ya nchi au awe serikalini au chama chochote cha siasa.

LAZARO MAMBOSASA – SACP

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAM.

09/03/2020

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kuhusishwa na kupewa sumu
- Mwakyembe mgonjwa; afya yake yadorora; ngozi yavimba mwili mzima

- Magufuli: Nikiwa Waziri nilinyweshwa sumu na viongozi waliochukia utendaji kazi wangu, nilitaka kujiuzulu
 
Back
Top Bottom