Nchi yetu, na hasa Jeshi la Polisi, kwa vitendo vyake, linadhihirisha kuwa halipo kwaajili ya kuutumikia umma, halipo kwaajili ya kusimamia sheria, wala kulinda haki za msingi za raia na binadamu kwa ujumla.
Nchi hii kumekuwa na matukio ya kishetani kabisa, matukio ya kuteka, kutesa na kuua watu, ambayo yamekuwa yakifanyika dhidi ya raia wasio na hatia yoyote kwa mujibu wa sheria za nchi. Washukiwa wakuu wa uovu huo, ambao wamekuwa wakinyoshewa vidole, kwa mtazamo wa wananchi wengi na ushahidi wa kimazingira wamekuwa ni Polisi na UVCCM.
Wakati watu wakiendelea kutekwa na kupotezwa, na vyombo vya usalama vikiendelea kunyoshewa vidole na wananchi, anatokea kiongozi mwandamizi wa Serikali, mkuu wa Wilaya, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya, na mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM ya wilaya, anatoka hadharani na kutamka kwa uwazi kuwa ushindi wa CCM wajati wa uchaguzi huwa hautokani na kura za wananchi bali kwa uharamia ambao Serikali huwa inafanya dhidi ya wapinzani huko maporini, halafu polisi wapo kimya!! Kama polisi hawahusiki kabisa na huo uharamia, na imekuwa ikinyoshewa vidole kuhusiana na huo uharamia, huyu aliyejitokeza wazi na kutamka kuwa yeye ni miongoni mwa maharamia hao wa kuwapeleka watu porini, bila shaka ni kuwateka, kuwaua na kuwatupa porini, Polisi si wangekuwa wamepata pa kuanzia? Mbona polisi wapo kimya? Au polisi huwa ni sehemu ya huo uharamia ambao wapinzani hufanyiwa huko porini ndiyo maana wanashindwa kuchukua hatua?
Na kuna yule kiongozi wa UVCCM mkoani Kagera, alitamka wazi, akiwaagiza polisi kuwa endapo kuna mtu yeyote atanayemkosoa Rais au Serikali atapotea, Polisi wasimtafute, akimaanisha kuwa wao UVCCM watakuwa ndio wamempoteza. Na kwa sasa kuna vijana viongozi wa BAVICHA na wanaharakati wametekwa na kupotezwa, kama Polisi siyo wahusika, na hawawajui wahusika wa huo ushetani wa kuteka watu, mbona huyu aliyetamka wazi kuwa ni mhusika, hajawahi kukamatwa na kuhojiwa mpaka leo?
Rais Samia amechukua hatua za kiutawala dhidi ya haramia aliyekuwa DC wa Longido. Ilitegemewa baada ya huyu bwana kuondolewa kwenye nafasi ya uongozi, vyombo vingine, ikiwa ni pamoja na polisi, vingefuatia katika kuchukua hatua dhidi yake, LAKINI cha ajabu, tunashuhudia hakuna hatua zozote?
Je, umma tuamini kuwa ushetani aliokuwa anaufanya aliyekuwa DC wa Longido, ulihusisha pia jeshi la polisi, ndiyo maana hawawezi kuchukua hatua? Je tuamini pia kuwa Polisi inafuata maagizo ya kiongozi wa UVCCM kuwa wakosoaji wa Serikali wakitekwa na kupotezwa Polisi hawatakiwi kuwatafuta kwa sababu ni CCM kupitia UVCCM ndiyo itakuwa imewateka na kuwapoteza?
kwa kweli kama Taifa tupo kwenye laana kuu, maana tuna Jeshi la Polisi ambalo lipo haraka sana kuchukua hatua dhidi ya watu wasio na hatia lakini lipo kimya dhidi ya uovu mkubwa kama wa upotezaji wa uhai wa binadamu? Je, wao ni washiriki katika uovu huo? Kama siyo washiriki, kwa nini wanashindwa kuchukua hatua dhidi ya uovu huu wa kuwateka na kuwaua raia huku kuna watu wanajitokeza na kutamka kuwa wao ni sehemu ya washiriki?
PIA SOMA: