Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 667
TAARIFA KWA UMMA
Baada ya uteuzi wa Wagombea wa nafasi za Uongozi katika nafasi mbalimbali za Serikali za Mitaa, kuna Chama cha Siasa kimepanga na kinahamasisha wafuasi wao kwa njia mbalimbali ikiwepo kukutana, kupigiana simu, kutumiana ujumbe na kwa kutumia makundi sogozi, kudhuru watu na kuharibu Ofisi za Serikali.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwafuatilia kwa karibu ili wakamatwe na hatua nyingine za kisheria zifuate.
Kupata matukio mengine ya kiusalama wakati wa uchaguzi bofya: LIVE - Uzi Maalum wa Matukio ya Kiusalama kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wafuasi wao kama wanaona kuna kasoro katika mchakato wa uteuzi wa wagombea wao, wafuate sheria na kanuni zinavyoelekeza na si kupanga na kuhamasishana kufanya uhalifu.
Aidha, linatoa onyo kali kwa yeyote anayepanga na kuhamasisha uhalifu wa aina hiyo kuacha mara moja.
Vinginevyo hatupo tayari kumvumilia mtu, kikundi cha watu au chama chochote cha Siasa kinachopanga uhalifu wowote ili kutaka kuvuruga amani ya nchi, kwani hatuta muonea muhali tutamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria za nchi.
Tuna wahakikishia wananchi kuwa, Jeshi la Polisi limejiimarisha vizuri kuhakikisha kuwa wanafanya shughuli zao za kujiletea maendeleo na kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika mazingira yenye amani, utulivu na usalama hivyo wasiwe na hofu ya aina yeyote.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi Dodoma, Tanzania.