Polisi: Faini milioni 5 mpaka 20 ukibainika kupekua simu ya mwenza wako

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
601
1,509
Mkuu wa Polisi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Selestin Luhende amewataka wanandoa kuacha kupekua simu za wenza wao ili kuepuka madhara yanayoweza kupatikana ikiwemo ugomvi unaoweza kuvunja ndoa pamoja na adhabu zinazoweza kutolewa kwa mujibu wa sheria.

Amesema pia endapo mwanandoa utabainika au kukutwa na hatia ya kupekua simu ya mwenza wako adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni faini ya Milioni tano mpaka Milioni ishirini au kifungo cha miaka mitano na wakati mwingine vyote kwa pamoja.

Luhende ameeleza hayo wakati akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya usalama katika kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa kikiendelea wilayani humo.

"Kupekua simu ya mwenza wako au kuangalia meseji zilizoandikwa ujue tayari umevunja sheria za nchi na ukipatikana na hatia adhabu yake ni Shilingi Milioni tano au Milioni Ishirini au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja" amesema OCD Selestin Luhende

Amesema endapo utampiga mwenza wako kwasababu ya kuangalia simu jambo la kwanza kushughulikiwa ni kupekua simu ya mwenza wako.
 
Kupekuwa simu haikwepeki inapobidi ili kupata evidence.
 
Huyo sio mke tena ikiwa huna uhuru wakutumia simu yake au kuitazama.
Nahili nibomu kubwa ambalo litatafuna vizazi hivi vya 2000 kwakua namigogoro mingi yandoa nazaidi ndoa nyingi kufa kabisa kwasababu ya vitendo vya usaliti ndani ya ndoa.
Kama taifa tutegemee single mother wengi sana navijana walio kwenda kiumri bila hata kuowa kabisa.
Kazi yao kuzalisha watoto wawatu nakuwaachia wazee wao mizigo mikubwa ya wajukuu na vitukuu.
 
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Selestin Luhende amewataka Wanandoa kuacha kupekua simu za Wenza wao ili kuepuka madhara yanayoweza kupatikana ikiwemo ugomvi unaoweza kuvunja ndoa pamoja na adhabu zinazoweza kutolewa kwa mujibu wa sheria.

OCD Luhende endapo Mwanandoa utabainika au kukutwa na hatia ya kupekua simu ya Mwenza wako adhabu yake kwa mujibu wa sheria ni faini ya Tsh. milioni 5 mpaka Tsh. milioni 20 au kifungo cha miaka mitano na wakati mwingine vyote kwa pamoja.

Luhende amesema hayo wakati akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya usalama katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikiendelea Wilayani humo “Kupekua simu ya mwenza wako au kuangalia meseji zilizoandikwa ujue tayari umevunja sheria za Nchi na ukipatikana na hatia adhabu yake ni Tsh. milioni 5 au milioni 20 au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja”

Amesema endapo utampiga Mwenza wako kwasababu ya kuangalia simu yake na kukuta jambo la kukukasirisha, jambo la kwanza kushughulikiwa ni kosa la wewe kupekua simu ya Mwenza wako.
 

Ukiona ndoa inaingiliwa hivi ujue kataa ndoa wana busara sana na ni wa kufuata! Mwanamke anapekuliwa kijirizisha, ila kamwe hatutoi ushahidi, ukisharizika wewe unataka Nani tena arizike? Unasepa!?
 
Hii ndio habari njema Pekee tangu mwaka huu uanze
 
DC ni simp kama simp wengine tu muscaline ni lazima ajue mwenendo wa mwanamke wake ili ujiepushe na mengi

No matter how much you trust your woman, go through her phone

Learn or perish
 
Kama wenza wanapekuliana viungo vya uzazi hadi wanapata watoto itakua simu! Afande ebu tuaache kwanza, na kila abiria achunge mzigo wake!!
 
Sababu kubwa ni kwamba kesi nyingi sana zinazokwenda Polisi chanzo ni simu

Hata Wachungaji wengi sikuhizi kwenye semina za Ndoa wanawaasa Wanandoa waaminiane na kuacha kuchunguzana simu zao
 
Inaonekana poti kachanganya vipengele vya Sheria ya Makosa ya Mtandao na Sheria ya Usalama wa Taifa bila kutoa ufafanuzi wa kutosha. Kila sheria ina mazingira yake ya utumiaji.

Adhabu aliyoitaja ya faini ya shilingi milioni tano hadi ishirini au kifungo cha miaka mitano si sahihi. Adhabu ya kosa la kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine chini ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ni faini isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu, au vyote kwa pamoja.

Mwamba ajitahidi asichanganye sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…