Mh Rais, salamu nyingi zikufikie.
Najua wewe sio member ila huwa unasoma sana JamiiForums na mengi umeyapata kupitia humu na kuyafanyia kazi.
Kuna jambo moja nataka uniondoe wasi wasi, hivi msimamo ni kutumbua majipu au kuyaondoa usoni na kuyaweka kwapani?
Kashfa nyingi zinazohusu jeshi la polisi mbali na uthibitisho usio na shaka,bado majipu yamehamishwa, kwanini yasiondolewe kabisa mwilini?
Kuhamisha jipu mara nyingi hugeuka kansa,jipu ni jipu dead cells zake hazifufuki.
Najua kuna watu wameondolewa nafasi za juu polisi sasa wapo mikoani,kuna watu wameondolewa mikoani wapo makao makuu ya jeshi,wengine wamehamishwa wilaya zao.
Naomba kama unatumbua tumbua kama unahamisha msamiati wa kutumbua achana nao kabisa maana utakupa umaarufu wa muda mfupi tu na dharau ya kudumu.
Najua mkuu wao anatumbua kwa huruma,uswahiba wake unamponza na amedangnywa sana na wawakilishi wake, hebu mwambie awe serious na jeshi letu. Kama polisi anakuwa mbadhirifu nani atakuwa muungwana?
Wapo waliopewa magari,fedha na nyumba wakati wa chaguzi,fukuza wote maana wamepoteza imani kwa askari wadogo.
Ipo siku utakumbuka ninachosema kama utatenda au itaacha.
Karibu Tanga utumalizie mgogoro wa Meya kama ilivyokuwa huko Dar.