Ndugu zangu hali ya kiusalama kwa sasa ni tete hapa nchini kwani kumekuwepo vitendo vingi vya uvunjifu wa Amani vinavyo fanywa na walifu hatari.
Huko Kagera juzi tuu magaidi wamezingira kijiji na kufanya uhalifu pamoja na kupora Mali za RAIA na kuwajeruhi. Interejensia ya polisi haikuweza kujua kutokea kwa uhalifu huo mpka umetendeka.
Ukiachilia mbali tukio hilo, lile gaidi hatari lililokuwa likishikiliwa na polisi huko Mwanza likihusishwa na mauaji ya msikitini na huko Tanga limetoroka mikononi mwa polisi na halijulikani liko wapi na linapanga uhalifu wapi.
Kwa hali kama hii sio busara kabisa kuruhusu mikusanyiko ya watu Kama jeshi la polisi lilivyo tangaza kwani hawa magaidi hupendelea sana kufanya uhalifu maeneo ambayo wanasiasa tu wanapo kusanyika na sio kwingineko.
Na tunashukuru Mungu haya magaidi kufanya uhalifu kwa wanasiasa tuu, maana wangekuwa wanashambulia hata mikusanyiko ya kidini au michezo tungeumia wengi sana. Tunaomba Mungu waendelee kushambulia mikusanyiko ya kisiasa tuu hivi hivi.
Kwahiyo nimeona maamuzi ya BAVICHA ya kuungana na jeshi la polisi kuzuia mkutano Wa cccm yamejaa uzalendo Wa kweli na wa kishujaa kwa taifa Lao. Jukumu la ulinzi Wa nchi hii ni letu sote BAVICHA wameonesha mfano tuwaunge mkono.
Tukiwaacha ccm wafanye mkutano haramu halafu wakavamiwa na magaidi sisi sote tutalaumiwa kwa kuto kuchukua hatua za kuzuia uhalifu kutendeka. Tusingependa wenzetu wayapate madhara kwani sisi ni ndugu na tunawapenda sana waendelee kuishi..
Ccm waelewe tuu BAVICHA pamoja na jeshi la polisi hawazuii mkutano wao kwa nia mbaya bali ni kulinda usalama wao na mali zao wakiwa kama RAIA wema.