Pole Marc Guehi umetuonesha madhumuni ya FA

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
3,260
5,256
Nyota wa timu ya taifa ya Uingereza Marc Guehi yupo kwenye hatihati na huenda akakabiliwa na mashtaka ya chama cha mpira cha FA kwa kuandika maneno 'Ninampenda Yesu' kwenye kitambaa cha mkononi cha manahodha wa vilabu vya kandanda Uingereza, kitambaa ambacho kilikua na alama ya upinde wa mvua kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.

1733301509454.jpg

Hii ilitokea kwenye mchezo wao dhidi ya Ipswich Town, ambapo Crystal Palace walishinda goli moja kwa sifuri. Kwa mujibu wa FA wachezaji hawaruhusiwi kuweka jumbe za kiimani na kidini, ila wameonesha kuwa unaweza kuweka jumbe zenye kuunga mkono mambo kama mapenzi ya jinsia moja na hata wengine utoaji wa mimba kuwa ni haki muhimu kwa wanawake.

KWA HILI FA MMEFELI SANA TENA MBALI!
 
pole sn mwamba marc...ila nao maostaz wengi wameyageuza madrassa kuwa gestiii mazeee ....wanakesha kutoboana spika mlee mazeee daah
 
pole sn mwamba marc...ila nao maostaz wengi wameyageuza madrassa kuwa gestiii mazeee ....wanakesha kutoboana spika mlee mazeee daah
Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amewasili Roma baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati ambapo alisema kuwa tabia ya baadhi ya mapadri Wakatoliki waliokuwa wakiwanyanyasa watoto wadogo kingono kanisani inaweza kulinganishwa tu na misa ya Mashetani.

Baba Mtakatifu alifanya ziara ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu wa imani tofauti katika eneo hilo na wachambuzi wengi wamesema kuwa imekuwa ya kufana.

Wengi wanasema kuwa Baba Mtakatifu kulinganisha vitendo vibaya vya ngono walivyofanyiwa watoto na mapadri na misa ya mashetani ni lugha nzito hasa ikitambuliwa kuwa tayari Papa Francis amewahi kuomba msamaha kwa vitendo hivyo kote duniani.

Vitendo hivyo vimeharibia sifa Kanisa Katoliki kwa muda mrefu sasa.

Taarifa kutoka makao makuu ya Papa yanasema kuwa kwa mara ya kwanza tangu yeye achukue wadhifa wake anatarajiwa kukutana na wale walionyanyaswa na mapadri kingono.

Wakatoliki wengi walikasirishwa na vitendo hivyo na wamefurahi kuwa Papa anaweza kuomba msamaha na kisha akutane na walioathirika na wengi wanasubiri kusikia atakachowambia atakapokutana nao.

Hata hivyo iwapo Papa anataka kuaminiwa zaidi itabidi awaadhibu wanaume waliofanya vitendo hivyo na wale Kanisani waliokuwa wakiwaficha waliofanya makosa hayo wanapaswa kuachishwa kazi Kanisani.
 
Ni ngumu kuamini kuwa ukristo unapinga ushoga, kwa kuwa huko kwa wakristo vitendo vinapigiwa upatu na serikali zao, makanisa na watu wa kawaida!
 
Ni ngumu kuamini kuwa ukristo unapinga ushoga, kwa kuwa huko kwa wakristo vitendo vinapigiwa upatu na serikali zao, makanisa na watu wa kawaida!
Vitendo hivi vinafanywa na viongozi wa kanisa hasa katoliki sasa watapinga vipi? Mtu demu zima unaambiwa usioe matokeo yake ndio haya
 
Back
Top Bottom