Leo ndio siku tunayohitimisha sherehe za Christmas, lakini pamoja na kuwa ni sherehe kuna watu imewaendea vibaya. Natoa pole rasmi kwa wafuatao
Kwa wale ambayo wameachwa mataa kwenye mtoko yaani mlipanga vizuri na mpz wako kuwa mtatoka wote,cha ajabu mda unafika ghafla mmoja anabadilika na kukutoroka..anaporudi ukimfatilia anakuwa mkali na kibaya zaidi unagundua alitoka na mwingine.
Pole kwa wale ambao walijiamini kuwa wanapendwa wao tu,lakini siku ya leo ndio wamegundua kuwa kumbe wako wengi.
Pole kwa wale waliobanwa hali walikuwa wameweka mchepuko tayari tayari, lakini wife naye akawa mjanja.
Pole kwa wale wanaume waliodiliki hadi kulipia chumba na cha ajabu yule mtarajiwa hakutiga
Pole kwa wale mliotoka safi ila cha ajabu mkakutana na x wako maeneo ya pamoja na moyo ukakuuma sana
Lakini pole kwa wale mlionusulika kufumaniwa au mlifumaniwa kabisa.
Pole kwa wale mlioamua kutoka wote ila ghafla mwenzio akakujibu hayuko vizuri ila muongee tu.
Na wewe ongeza za kwako tukupe pole.