johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 96,236
- 168,802
Waziri mkuu mh Majaliwa amesema Vyama 6 vya Siasa vyenye Sifa ya kupata Ruzuku ya Serikali vimepokea Jumla ya tsh 17.5 bilioni
Vyama hivyo sita ni Chadema, ACT wazalendo, NCCR mageuzi, CUF, CCM na DP
Chanzo: Swahili Times
Nawatakia Juma Takatifu Lenye Baraka tele!
---
Katika bajeti ya 2022/23, Serikali imetoa ruzuku ya Sh17 bilioni kwa vyama sita vya siasa vyenye sifa za kupewa ruzuku.
Vyama hivyo ni CCM, Chadema, NCCR- Mageuzi, ACT Wazalendo DP na CUF na kwamba itaendelea kufanya hivyo ikiwa ni takwa la kisheria.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Jumatano Aprili 5, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akisoma hotuba ya Makadilio ya Mapato na matumizi kwa Ofisi na Wizara zilizo chini yake
Kwa kauli hiyo, ni dhahiri kuwa imehitimisha minong'ono ya Chadema kuwa hawajachukua ruzuku kutoka Serikali.
Kwa muda sasa kumekuwa na mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Chadema ambao walishakaririwa mara kadhaa wakisema hawachukui ruzuku ingawa siku za hivi karibuni wamekuwa kimya kuhusu jambo hili.
Waziri Mkuu hakusema vyama hivyo kila kimoja kimechukua kiasi gani cha fedha kwa wakati huu.
Waziri Mkuu amesema demokrasia imeendelea kuimarika nchini ikiwemo uhuru wa vyama vya siasa na nyombo vya habari katika kujenga nchi yao.
MWANANCHI