- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Salaam Wakuu
Nimekutana na picha hii ya uwanja uliojaa sana watu kupitiliza, je ni picha ya kweli au masuala ya AI haya?
Nimekutana na picha hii ya uwanja uliojaa sana watu kupitiliza, je ni picha ya kweli au masuala ya AI haya?
- Tunachokijua
- Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia TinEye umetupa majibu yanayoonesha kuwa Picha hii ya uwanja uliojaa watu ni halisi, na ilipigwa mnamo Julai 17, 1994, katika Uwanja wa Rose Bowl, ambao uko mjini Pasadena, California.
Picha hiyo ilipigwa wakati mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 1994, kati ya Brazil na Italia. Mchezo huu ulimalizika kwa sare ya 0-0 baada ya dakika 90 za kawaida na dakika 30 za nyongeza. Brazil ilishinda fainali hiyo kwa mikwaju ya penalti 3-2, na hivyo kutwaa taji lao la tano la Kombe la Dunia.
Zaidi ya hayo JamiiCheck imepitia Tovuti rasmi ya FIFA na vyanzo vingine ambavyo pia vinaelezea mchezo huo na kuonesha picha hizo. Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa katika mchezo huo wa fainali la Kombe la Dunia kati ya Brazil na Italia watu 94,194 waliingia kushuhudia mchezo huo, soma hapa na hapa.