Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,515
- 4,016
Picha ya jeraha la Ibrahim Abdallah Hamad a.k.a Ibra Bacca, beki kisiki na tegemeo ndani ya kikosi cha yanga yashtua wengi ikiwa zimesalia siku takribani mbili tu kuelekea Oktoba 19 kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo utakao wakutanisha na Simba SC.
Bacca ali-share picha hii Instagram (insta story) ikionesha kifundo cha mguu kikiwa kimevimba, jeraha ambalo alilipata kwenye mechi dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo ya kufuzu AFCON 2025 huko Morocco ambayo Taifa Stars ilipoteza kwa bao 2-0.
Taarifa ya Walter Harrison, Meneja wa kikosi cha Yanga ilibainisha kuwa "Wachezaji wote waliokua kwenye majukumu ya timu za Taifa wapo vizuri, hakuna taarifa mpya kuhusu majeraha zaidi ya Farid Mussa ambaye ameanza mazoezi mepesi, wengine wote wapo sawa"
Kumbe hii ya Ibrahim Bacca ni danganya Toto! Simba msiingie kwenye mtego huo!
Kumbe hii ya Ibrahim Bacca ni danganya Toto! Simba msiingie kwenye mtego huo!