Picha X-rays kali za kutisha ambazo ni ngumu kuamini

mcTobby

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
4,274
12,589
Maisha ni safari ya ajabu, Hizi picha hapa chini sio za kuchora, ni matukio halisi yaliyotokea.
1. Mwaka 2020, msichana mmoja alipata ajali mbaya akiwa ndani ya gari huku miguu yake ikiwa juu ya dashboard.

Ajali ilipotokea, mguu wake ulisukumwa kwenda nyuma vibaya na hii ni picha ya X-ray ikionesha jinsi alivovunjika vibaya sana
20250328_200518.jpg


2. Jamaa alipata ajali mbaya baada ya mkono wake kunaswa kwenye mashine ya kusaga nyama. Picha ya X-ray inaonesha namna mifupa imevunjika kila upande na huko mkono wake ukiharibika vibaya sana.
20250328_200529.jpg


3. Chen Liu, kijana wa miaka 27, alipatikana amekufa kwenye mabwawa ya matope karibu na Sydney, Australia. Picha za X-ray zilionesha amepigwa misumari 34 mwilini na muuaji wake ikiwa ni unyama uliopitiliza.
20250328_200537.jpg

4. Mzee Leroy Luetscher alianguka juu ya mkasi wa kukatia maua na matawi. Mkasi ulimchoma kwenye jicho hadi shingoni. Licha ya maumivu, aliweza kupiga simu kuomba msaada. Na Mungu si Athumani, Madaktari walimwokoa jicho lake na maisha yake.
20250328_200547.jpg

5.5. Jamaa mmoja kutoka Korea Kusini alikuwa anajisikia maumivu ya kichwa yasiyoisha. Alipopelekwa hospitali mwaka 2004, madaktari waligundua X-ray inaonesha msumari wa sentimita 5 kichwani mwake. Inaaminika aliupata kwenye ajali miaka minne nyuma bila kujua.


20250328_200552.jpg


6. Hii X-ray inaonesha jinsi kiwiko cha mtu kilivyoharibiwa vibaya baada ya kupigwa risasi kwa bunduki aina ya 12-gauge shotgun. Ukiangalia vizuri sehemu hio ilitawanyika vibaya sana..
20250328_200559.jpg


7.Dogo mmoja huko London alidakwa akiwa anaiba na baadae alichomwa kisu cha inchi 5 kichwani. Cha ajabu ni kwamba aliweza kuishi, hii X-ray inaonesha kisu kilivyopenya kwenye fuvu lake.
20250328_200606.jpg

8.Isidro Mejia, fundi ujenzi, alichomwa na misumari sita kichwani baada ya mashine ya kupiga misumari kulipuka. Misumari mitano ilitolewa siku hiyo hiyo, na mmoja ulisubiri uvimbe upungue. Kwa miujiza ya Mungu alinusurika kifo
20250328_200647.jpg



9.Mwaka 2019 huko Iraq, kulikuwa na maandamano ambaye kulitokea vurugu, kijana mmoja alipigwa tear gas canister moja kwa moja kichwani, Iliingia hadi kwenye fuvu na kusababisha kifo chake papo hapo, na hii ndio X-ray yake
20250328_200659.jpg

10.Mchina mmoja alilazimika kwenda hospitali baada ya kuanza kupata maumivu makali ya tumbo. Alipoulizwa chanzo cha maumivu, alisema hajui kilichosababisha.

Baada ya madaktari kumpiga X-ray na kumuonesha picha, alikiri kuwa aliingiza chupa ndani ya mwili wake na alipojaribu kuitoa kwa waya, ikazidi kuzama.
20250328_200707.jpg

11.Jamaa mmoja aliingiza vibrator kwenye njia ya haja kubwa, ikakwama. Badala ya kwenda hospitali moja kwa moja, aliamua kujitoa mwenyewe kwa kutumia kijiko cha kubania mboga, nacho pia kikakwama humo humo.
20250328_200718.jpg


12.Jamaa mmoja kutoka Mexico alipanga kumvisha pete mpenzi wake kwa njia ya kipekee, akaificha ndani ya milkshake. Cha kusikitisha, badala ya kuikuta mdomoni, demu aliimeza kabisa bila kujua.

20250328_200734.jpg



credit to @kingpablotz pale mjini X.
 
Back
Top Bottom