Picha: Wafuatao ni samaki tunaowapata sana hasa ukanda huu wa Lindi beach

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,286
50,365
Mnaoishi bara Poleni sio kidogo endeleeni kutunyima protein ya nyamaPori, senene na kumbikumbi. Tunaokaa pwani ya Bahari Hindi tunaendelea kufaidi sea food.
Kibua-huyu najua maarufu sana hasa Kwa dar
Changu-huyu Lindi na Mtwara Kwa wingi
Lupapa
Chewa - huyu wa supu kabisa moja ya samaki mwenye bei nzuri watoto wa kivinje na Mchinga wanaelewa
Kipepeo - huyu hata mimi mwenyewe Sina maelezo yake mengi sana sijawahi kumla
Pronzi sijui nimwite bronzi - jamii ya kambakochi na mwenyewe wakubwa bei yake nzuri
Dagaa mchele-wa buku waliokaangwa unakula na ugali na maji ya baridi
Kolekole-kilwa na somanga Safi Sana
Ngisi - mtoa wino huyu na pweza unamkubali yupi?
Kiatu - huyu samaki Kiatu hana nyama nyama chembamba

WOTE WAKO PICHANI HAPO
DSC_0248.JPG

DSC_0245.JPG
 
1. Bunju
Huyu mtamu sana ila anayo sumu ya hatari
2. Kikande
Huyu anachunwa kama ng'ombe mtamu kama kuku
3.Puju
Huyu ana pua kama nguruwe
4.Jodari
Huyu ana mnofu rangi ya damu ya mzee
5.Pono
Huyu ana mdudu kichwani ukimla huyo mdudu utalala usingizi wa pono
6. Mkizi
Huyu anavutia kwa uzuri wake wa kung'aa ila hana ladha hata kidogo
7. Saladini
8. Mbuzi bahari
9. Tili
Huyu ana mdomo umechongonga kama sindano 10. Msusa
11. Changu
12. Taa
Huyu mnofu wake kama una mchanga mchanga laini usio kera na unalika vzr tu
13. Tasi
Huyu hana magamba ni mtamu sana
14. Chongoe 15. Barakuda 16. Mzira
Huyu ni mrefu hata akiwa mdogo
17. Mnendele
Huyu anamiba ya kutosha
18. Lumbunga
Huyu ni dagaa ni mtamu kuliko dagaa mchele
19. Mkunga
Huyu yupo kama nyoka
20. Kasa
Huyu ni kobe bahari nyama yake tamu sana hasa kwa pilau lkn ukikutwa na nyama yake lazma uisaidie polisi ktk kazi zao

wengne nitaongezea baadae
 
na.19 Mkunga,
Sura yake na umbile kama nyoka.Wako wa rangi nyingi sana na hata makabila.Wana mafuta sana na ni wazuri kwa kupata harufu nzuri kwenye mchuzi.Tatizo hawana nyama.Sehemu kubwa ni miba.Kinofu kidogo utakachokipata na ukakichoma kwa mkaa utafurahi sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom