Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,299
- 6,314
Viongozi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Kanda ya Kati na Mkoa wa Dodoma wamefika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kumjulia hali Mwenezi wa BAWACHA Taifa, Bi. Sigrada Mligo, ambaye amelazwa hospitalini hapo baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Mkoa wa Njombe.
Bi. Sigrada alidaiwa kushambuliwa na mlinzi wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, John Heche, tukio ambalo limezua mjadala mkubwa ndani na nje ya chama hicho. Viongozi wa BAWACHA waliotembelea hospitalini hapo wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliohusika.
"Viongozi wa BAWACHA Kanda ya Kati na Mkoa Dodoma wamefika Hospitali ya Benjamini Mkapa Dom kumjulia hali Mwenezi wa BAWACHA Taifa Bi Sigrada Mligo aliyelazwa hapo akihamishwa kutoka Hospitali ya Mkoa Njombe baada ya Kupigwa na Mlinzi wa Makamu Mwenyekiti Chadema Taifa John Heche." - amwandia Yericko Nyerere
Pia, Soma

- Ghasia Ndani ya CHADEMA: Mwenezi wa BAWACHA Taifa ashambuliwa na Walinzi wa Heche
- Katibu wa Siasa na Uenezi Njombe: Amjulia hali Katibu Mwenezi BAWACHA Taifa Sigrada Mligo