Mamujay
Senior Member
- Dec 24, 2022
- 149
- 344
PICHA NA VIDEO ZA WAHUBIRI WAKIWA WANAOMBA PORINI NI UTAPELI MTUPU!
Wahubiri matapeli wana tabia ya kupiga picha na kuchukua video wakiwa porini au milimani.Kisha huzirusha kwenye mitandao au television.Nia yao kubwa ni kuwaaminisha wasaka miujiza wasio na maarifa ya Neno la Mungu,kuwa wao ni waombaji kabambe.
Huenda porini na milimani na kujirekodi eti wanatafuta sana upako kwa maombi yao.Kisha baada tu ya kurusha hizo picha na video; wanatoa vitu vipya vya upako na kuwauzia wagonjwa na watafuta miujiza ya maisha.Hili ni jambo la kishetani na linapingana na Neno la Yesu Kristo.
Soma{ mathayo 6:5-6 Tena msalipo,msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na ktk pembe za njia,ili waonekane na watu.Amin,nawaambia,wamekwisha kupata thawabu yao.Bali wewe usalipo,ingia ktk chumba chako cha ndani,na ukiisha kufunga mlango wako,usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi }.
Maombi ya kweli na yenye nia njema yanapaswa kuwa ya siri kati ya mhubiri na Mungu.Hivyo ninyi mbumbumbu wasaka miujiza na hamtaki Neno la Mungu; huku duniani mtaumizwa sana na hao mbwa mwitu wakali,waliovalia mavazi ya kondoo.Ni upumbavu na utumwa wa kishirikina kuishi na vitu vya upako.Wakristo wa kweli kamwe hawatumii vitu vya upako.Neno la Mungu linatosha.
Yesu Kristo wala mitume na manabii hawakuagiza kanisa la Mungu litumie vitu vya upako kutatua matatizo na changamoto za maisha.Haya ni mambo ya ufunuo wa kishetani na ni njia za kitapeli za kuvuna pesa kwa wenye akili kama za nyumbu makanisani.
Nimetumwa kufungua akili na fikra za watu duniani.Nanyoosha rula kwa mambo ya kishenzi ktk mwili wa Kristo duniani.
By mtumwa wa Kristo pastor Mfinanga.+255766259983.