Picha: Huyu Rais wa Croatia ni Gwiji wa Diplomasia na Marketing. Ni Hatari !!

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,629
34,192
Michuano ya kombe la dunia imemalizika wikiendi iliyopita nchini Urusi baada ya kushuhudia timu ya taifa ya Ufaransa ikiibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4 – 2 dhidi ya Croatia.

8f85d1c01fbc3821706b59a63bd87a9456f5acfe-tc-img-preview.jpg

Licha ya ukubwa wa mechi hiyo lakini kinachoendelea kuzungumzwa ni namna rais wa Croatia, Kolinda Grabar Kitarovic alivyokuwa karibu mno na rais Ufaransa, Emmanuel Macron huku wakionekana kama wapenzi hali iliyokuwa kivutio kikubwa machoni mwa wafuatiliaji wa fainali hiyo.
MACRON-2-e1531752474285.jpg

Rais huyo wa Croatia, Kolinda Grabar Kitarovic ameitawala myoyo ya watu wengi kufuatia tukio hilo kwenye mchezo wa fainali jijini Moscow hali inayopelekea watu wengi kwenyemitandao kutamani kuona wawili hao wakiwa kwenye mahusiano.
kolinda-6-1.jpg-1-1.jpg

Wakati mchezo huo ukiendelea wengi walidhani Kolinda ni Mke wa rais huyo wa Ufaransa, Macron mwenye umri wa miaka 40 ilihali mkewe ni Brigitte mwenye miaka 65.
dc-Cover-irn8r4rvfsav94ntpddhjg3he3-20180717103344.Medi_.jpeg

Kolinda ameolewa na mchambuzi wa maswala ya usalama, Jakov Kitarović tangu mwaka 1996 huku wakiwa wamejaaliwa kupata watoto wawili.
22e86c4f0fa2ec700ebf94c1403a51772a6e871f-tc-img-preview.jpg


Mama huyo rais wa Croatia alionekana akimkumbatia Macron muda wote na hata wakati wakiwa uwanjani kugawa tuzo wawili hao hawakuhitaji miavuli mvua ilipokuwa ikinyesha.

e4e5e56ae8916f92ee2965e0812adfd3177d5e95-tc-img-preview.jpg


Wengi wameuliza sababu za rais huyo wa Croatia kuwa mwenye furaha muda wote wakati timu yake ikiwa imepoteza dhidi ya Ufaransa je imetokana na taifa lake kutinga fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza au marafiki wakaribu aliyokuwa nao siku hiyo.

a8ee9af1101e77efe82b02d5569e8dafa214b60b-tc-img-preview.jpg

Grabar Kitarovic ameonekana akiwakumbatia wachezaji wote bila kubagua na kuwapa pongezi kwa kazi nzuri waliyoonyesha uwanjani.

b87968816b7d3ce14dac426941b3020f9909bc75-tc-img-preview.jpg

Mama huyo mwenye watoto wawili, Grabar Kitarovic amehudhuria michezo yote ambayo taifa lake limecheza isipokuwa moja wa nusu fainali dhidi ya Uingereza kutokana na kuwepo kwenye kikao cha NATO huko Brussels.
17621041644876963002.jpg


Master.jpg


Source: Ukaribu wa Rais wa Croatia na Ufaransa wazua gumzo duniani (+Picha) - Bongo5.com

MY OWN OPINION:

Yaani Ufaransa wamechukua kombe la Dunia lakini kimya, Croatia mpaka leo imebaki kuwa gumzo. Huko Twitter inatrend kuliko kawaida, nadhani sasa kila mtu anaijua hii nchi. Wale wazee wa kuzurula tuambizane VISA inapatinaje mazee !!!!
 
Hata mimi ningependa kujua vivutio vinavyopatikana huko, ukimtoa huyo dada yangu Raisi nataka nijue fursa nyengine.
 
Kwa kweli inatia moyo unapoona unachezea nchi yako na rais wako yupo uwanjan kuwasapoti.
 
Unaambiwa huyu mama ni komandoo na amewahi kuongoza vikosi vya NATO kwa mafanikio makumbwa
Cheo chake cha kijeshi ni nini maana kuwa komando na kama huna rank huwezi Sema eti uliongoza vikosi kwa mafanikio. Alikua kanali au major
 
John Pia si alikuwepo Siku ya Simba Na Kagera
Baada ya Mechi akaanza kuporomosha matusi Eti Tundu limetobolewa, Tundu linatobolewa vipi wakati tayari Ni kitobo
Mzee ana matusi yule si mchezo.

Ipo siku atatukana mtu mse.ngee hadharani
 
Mbona ndo maisha ya wazungu? Kiss n hug ni vitu vya kawaida. Kwetu waafrica ndo inakuwaga issue kuuubwa!!!
 
Back
Top Bottom