Taarifa iliyotolewa na mamlaka ya udhibitui wa huduma za nishati na maji (EWURA) inaonesha kwanzia leo September 4, 2024 zimeshuka katika mikoa yote nchini. sababu za kushuka kwa bei yaPetroli na dizeli imetajwa kua ni kushuka kwa gharama za soko la dunia.
Taarifa inasema kwanzia leo Septemba 4 petroli inayochukuliwa Bandarini Dar es salaam imeshuka kutoka Tsh3231 kwa lita moja paka Tsh 3240. kwa bandari ya Tanga petroli imeshuka kutoka Tsh3,229 paka 3,142.
Kwa upande wa dizeli kwa bandari ya Dar es salaam imeshuka kutoka Tsh3,138 paka 3,011. Kwa bandari ya Tanga dizeli imeshuka kutoka Tsh 3,138 paka3,020. Na kwa bandari ya Mtwara kutoka 3,140 paka 3,021 kwa lita.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk James Mwainyekule, imetajwa mwenendo wa bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia kushuka kua miongoni mwa sababu ya kupaa kwa bidhaa hizo muhimu kwa uchumi.