Peter Msigwa ni mlaji wa matapishi yake

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,233
1,811
Peter Msigwa Mlaji wa matapishi yake

Uamuzi wa Peter Msigwa kuhama kutoka Chadema kwenda CCM unaacha alama mbaya katika siasa za Tanzania. Ni tukio linalofungua mjadala kuhusu uaminifu, uadilifu, na misingi ya uongozi. Msigwa, aliyewahi kuwa kiongozi mashuhuri ndani ya Chadema, sasa anaonekana kama kiongozi aliyeshindwa kuhimili changamoto na kushikilia misingi ya chama chake. Hii ni fundisho kwa viongozi wengine kwamba uaminifu na uadilifu ni muhimu zaidi kuliko madaraka, na kwamba kiongozi bora ni yule anayesimama imara katika misingi na itikadi zake, bila kujali ugumu wa hali. Wanachama na wafuasi wa Chadema wanapaswa kuendelea kushikilia misingi ya chama na kuwapinga wale wanaosaliti kwa maslahi binafsi

1. Kula Matapishi Yake Mwenyewe

Peter Msigwa alishawahi kusema hadharani kwamba, endapo angehama Chadema, basi nyumba na mali zake zichomwe moto. Kauli hii ilionesha kiwango cha kujitolea na uaminifu wake kwa Chadema. Leo hii, kwa kuhama kutoka Chadema na kujiunga na CCM, Msigwa amekula matapishi yake mwenyewe. Hii ni ukosefu wa msimamo na uaminifu kwa maneno yake mwenyewe. Kula matapishi ni jambo linaloonekana kwa waoga tu; wale ambao hawawezi kusimama imara katika misingi na maamuzi yao, hasa wakati wa changamoto

2. Akili Ndogo na Kukosa Uvumilivu

Msigwa amedhibitisha kuwa yeye ni akili ndogo. Akili kubwa huwa na uwezo wa kuhimili changamoto zote nyakati zote, bila kujali ugumu wa hali. Katika maisha ya kisiasa, changamoto ni sehemu ya kawaida, na kiongozi mwenye akili kubwa anajua jinsi ya kuvuka vipingamizi bila kuhatarisha uaminifu na itikadi zake. Kuhama kwake Chadema kwa sababu ya kukosa nafasi ya uongozi inaonesha wazi kuwa alikosa uvumilivu na ujasiri wa kukabiliana na changamoto hizo

3. Usaliti kwa Watu wa Iringa

Kuhama kwa Msigwa ni usaliti mkubwa kwa watu wa Iringa waliomchagua na kumwamini kama kiongozi wao. Usaliti ni kitu kibaya mno kwa binadamu, kwani unavunja imani na uaminifu ambao umejengwa kwa muda mrefu. Wananchi wa Iringa walimtegemea Msigwa kwa kuwa alikuwa sauti yao, mtetezi wa haki na maendeleo yao. Kuhama kwake kunawaacha wananchi hawa wakiwa na hisia za kukatishwa tamaa na kuhisi kusalitiwa,

4. Kukosa Uadilifu na Uaminifu

Msigwa amekosa uadilifu na ni wazi hata huko CCM hatoaminika. Alikuwa ndani ya Chadema kwa kuwa alikuwa kiongozi, lakini ameshindwa kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kupoteza nafasi za uongozi. Hii inaonesha kuwa uaminifu wake kwa Chadema ulikuwa wa juu juu na ulitokana na maslahi binafsi ya madaraka. Uchu wa madaraka, ulafi na ulevi wa madaraka ni tabia zinazoonesha kiongozi asiye na msimamo na asiyeaminika. Wananchi na wafuasi wa Chadema walimwamini Msigwa kama kiongozi mwadilifu, lakini hatua yake ya kuhama inaonesha kuwa alikuwa na ajenda za kibinafsi zaidi kuliko maslahi ya watu

5. Kukosa Busara na Hekima

Msigwa amekosa busara na hekima. Angeweza kukaa kimya baada ya kuondoka Chadema, lakini kuanza kuukejeli Chadema ni kiwango cha juu cha upumbavu na upofu. Kiongozi mwenye busara na hekima anajua kwamba ni bora kuondoka kwa heshima bila kushambulia chama ambacho kilimlea na kumkuza kisiasa. Kejeli na maneno ya kukashifu yanayotolewa na Msigwa baada ya kuhama Chadema yanaonesha ukosefu wa heshima na unyenyekevu. Hii ni tabia inayovunja moyo na kuonesha kwamba hajafikiria kwa kina kuhusu athari za maneno na matendo yake kwa wafuasi na wanachama wa Chadema

Nanyaro EJ
 
Msigwa anamaanisha hata huko ccm alikotimkia ikiwa hatapewa cheo chochote basi atakimbia vilevile, kwamba yeye hawezi kuishi bila cheo!.
Ingawa ni haki yake kikatiba kuhama kutoka CHADEMA kwenda CCM lakini kwakweli sababu za kuhama kwakwe (kwa mtu makini) hazina mashiko hata chembe!.
 
Ni mtu mzuri ila tamaa ya cheo inafuta mazuri yake yote.
 
Tulitegemea kauli za kipumbavu kama hizi zako toka kwa nyumbu wa CHADEMA. Nyie mtu kuhama chama ni kosa la jinai na sio haki ya kikatiba. Hiyo katiba mpya mnayotaka haitatoa uhuru wa mtu kuhama CHADEMA? Wewe Nanyaro ni CHADEMA mchana ila usiku ni CCM. Bora Mdude ambaye kajitoa ufahamu kuliko nyie mandumilakuwili ambao mko kotekote.
 
Alichofanya msigwa ni kitu ambacho mtu yeyote mwenye akili angekifanya.

1. unashuhudia mtu mmoja tu kuwa mwenyekiti wa maisha wakati wapo wasomi na wenye akili na uwezo kuliko yeye.

2. unashuhudia mtu analamba asali, anatokea gerezani hadi ikulu na ananyamaza kimyaaa. kama sio yule wa awali kabisa.

3. unashuhudia unyama kwa chacha wangwe.

4. unashuhudia usaliti kumpokea lowasa na sumaye na namna dr slaa alivyoondoka.

5. unashuhudia ukabila kwenye chama.

6. unashuhudia Mrema na timu yake wamekuja eneo lako la kugombea uenyekiti nyasa, anakunywa pombe pamoja na mpinzani wako nadi saa sita usiku, unapiga kelele mwenyekiti wako kimyaaa, na inasemekana mwenyekiti kaagiza wewe ndio uchinjiliwe mbali kwenye kinyang'anyiro.

7. wajumbe wawili waliotakiwa kupiga kura hawajapiga ili wewe ushindwe.

8. uchaguzi unaisha, unalalamika, lakini kimyaaa kwa king mbowe.

9. na siri nyingii ambazo anazo atazimwaga wakati wa kampeni mwakani.

10. Tundu Lisu hana hata gari wakati yeye ndiye mpiganaji mkuu kuliko hata mbowe, hadi anachangiwa kununua gari, hata mbowe hapigi changizo wakati kuna pesa kibao za ruzuku kutokana na covid 19.

kwa kifupi, hata Tundu Lisu, anakosa tu pa kwenda, amekichoka chama, amemchoka mbowe, amechoka ukabila. kungekuwa na chama kingine nje ya ccm, Tundu Lisu angeshaenda kitambo sana. na Tundu Lisu naye, ni mwanadamu, naamini uzalendo utamshinda muda si mrefu, atajiunga na ccm kwasababu hana chama kingine kwa sasa, chadema imemwacha kama anapambana peke yake na mwenyekiti inaonekana zile asali huwa hamgawii.

hivi ungekuwa wewe ndio msigwa, ungefanya nini?
 
alichofanya msigwa ni kitu ambacho mtu yeyote mwenye akili angekifanya.

Kila mtu aende akale kule aliko peleka mboga .
 
Hivi kataja sababu zipi za kuhamia CCM? Intelligence ya Chadema kumbe iko imara kiasi hiki. Hongereni, mko vizuri.
Hata haeleweki ila inafahamika kwamba kalipwa, lakini ccm wanawezaje kumnunua aliyeshindwa?
 
Peter Msigwa Mlaji wa matapishi yake

Uamuzi wa Peter Msigwa kuhama kutoka Chadema kwenda CCM unaacha alama mbaya katika siasa za Tanzania. Ni tukio linalofungua mjadala kuhusu uaminifu, uadilifu, na misingi ya uongozi. Msigwa, aliyewahi kuwa kiongozi mashuhuri ndani ya Chadema, sasa anaonekana kama kiongozi aliyeshindwa kuhimili changamoto na kushikilia misingi ya chama chake. Hii ni fundisho kwa viongozi wengine kwamba uaminifu na uadilifu ni muhimu zaidi kuliko madaraka, na kwamba kiongozi bora ni yule anayesimama imara katika misingi na itikadi zake, bila kujali ugumu wa hali. Wanachama na wafuasi wa Chadema wanapaswa kuendelea kushikilia misingi ya chama na kuwapinga wale wanaosaliti kwa maslahi binafsi

1. Kula Matapishi Yake Mwenyewe

Peter Msigwa alishawahi kusema hadharani kwamba, endapo angehama Chadema, basi nyumba na mali zake zichomwe moto. Kauli hii ilionesha kiwango cha kujitolea na uaminifu wake kwa Chadema. Leo hii, kwa kuhama kutoka Chadema na kujiunga na CCM, Msigwa amekula matapishi yake mwenyewe. Hii ni ukosefu wa msimamo na uaminifu kwa maneno yake mwenyewe. Kula matapishi ni jambo linaloonekana kwa waoga tu; wale ambao hawawezi kusimama imara katika misingi na maamuzi yao, hasa wakati wa changamoto

2. Akili Ndogo na Kukosa Uvumilivu

Msigwa amedhibitisha kuwa yeye ni akili ndogo. Akili kubwa huwa na uwezo wa kuhimili changamoto zote nyakati zote, bila kujali ugumu wa hali. Katika maisha ya kisiasa, changamoto ni sehemu ya kawaida, na kiongozi mwenye akili kubwa anajua jinsi ya kuvuka vipingamizi bila kuhatarisha uaminifu na itikadi zake. Kuhama kwake Chadema kwa sababu ya kukosa nafasi ya uongozi inaonesha wazi kuwa alikosa uvumilivu na ujasiri wa kukabiliana na changamoto hizo

3. Usaliti kwa Watu wa Iringa

Kuhama kwa Msigwa ni usaliti mkubwa kwa watu wa Iringa waliomchagua na kumwamini kama kiongozi wao. Usaliti ni kitu kibaya mno kwa binadamu, kwani unavunja imani na uaminifu ambao umejengwa kwa muda mrefu. Wananchi wa Iringa walimtegemea Msigwa kwa kuwa alikuwa sauti yao, mtetezi wa haki na maendeleo yao. Kuhama kwake kunawaacha wananchi hawa wakiwa na hisia za kukatishwa tamaa na kuhisi kusalitiwa,

4. Kukosa Uadilifu na Uaminifu

Msigwa amekosa uadilifu na ni wazi hata huko CCM hatoaminika. Alikuwa ndani ya Chadema kwa kuwa alikuwa kiongozi, lakini ameshindwa kuendelea kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kupoteza nafasi za uongozi. Hii inaonesha kuwa uaminifu wake kwa Chadema ulikuwa wa juu juu na ulitokana na maslahi binafsi ya madaraka. Uchu wa madaraka, ulafi na ulevi wa madaraka ni tabia zinazoonesha kiongozi asiye na msimamo na asiyeaminika. Wananchi na wafuasi wa Chadema walimwamini Msigwa kama kiongozi mwadilifu, lakini hatua yake ya kuhama inaonesha kuwa alikuwa na ajenda za kibinafsi zaidi kuliko maslahi ya watu

5. Kukosa Busara na Hekima

Msigwa amekosa busara na hekima. Angeweza kukaa kimya baada ya kuondoka Chadema, lakini kuanza kuukejeli Chadema ni kiwango cha juu cha upumbavu na upofu. Kiongozi mwenye busara na hekima anajua kwamba ni bora kuondoka kwa heshima bila kushambulia chama ambacho kilimlea na kumkuza kisiasa. Kejeli na maneno ya kukashifu yanayotolewa na Msigwa baada ya kuhama Chadema yanaonesha ukosefu wa heshima na unyenyekevu. Hii ni tabia inayovunja moyo na kuonesha kwamba hajafikiria kwa kina kuhusu athari za maneno na matendo yake kwa wafuasi na wanachama wa Chadema

Nanyaro EJ
Career politician. Hana kazi maalum ya kufanya na anategemea siasa kuishi. Njaa imemkaba.
 
Acheni watu wafanye maamuzi wanayoona yanawafaa , msilazimishe mitizamo ya watu ikawa Sana, by the CDM siyo kwamba ni chama Bora Sana kiasi kwamba mtu akiondoka kuna Jambo kubwa Sana la maana analipoteza. Period
 
Je ndani ya Chadema ni safi? Rufaa yake mngeisikiliza na kuitolea maamuzi ingeleta maana. Mbowe naye asifanye CDM chama cha familia itamtesa sana vinginevyo aachie ngazi. kwani CDM haina succession plan km chadema ya Bob Makani na Mtei. Imepoteza misingi yake
 
Hii ni sawa, wewe mwanaume ikatokea bila kujua ukamwoa mwanamke malaya, ukamjali kwa kila kitu kwa sababu alikuonesha mahaba uliyoamini ni ya kweli, lakini baadaye ukaona hitilafu, ukampunguzia majukumu. Lakini mwanamke huyu alichokuwa akikitafuta kutoka kwako ilikuwa ni umaarufu na pesa iliyotokana na majukumu uliyokuwa umemwachia. Mwanaume mwingine akamshawishi kwa ahadi nyingi, naye akaamua kukuacha, akamwendea huyo mwanaume mwingine aliyemvutia kwa ahadi kemkem. Huyu aliyemchukua mwanamke wa namna hii asijifariji kuwa anapendwa zaidi. Siku akipatikana mwanaume atakayeweza kumhadaa zaidi, atamwacha na wewe pia.

Msigwa ameenda CCM kufuata madaraka. Akipewa madaraka, CCM watahadaika na kuamini Msigwa anaipenda CCM, tena kwa kiwango zaidi ya makada walioko CCM miaka yote. Siku Msigwa atakapokosa madaraka, ndipo mapenzi yake kwa CCM yatakapoisha. Au hata wakimwacha miaka kama 3 hivi bila madaraka, ndipo watajua Msigwa alifuata nini CCM.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom