figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,772
- 56,224
Kuna kila dalili za aliyekuwa Mbuge wa Iringa, Mwenyekiti Kanda ya Nyasa na Mjumbe wa Kamati kuu na Mkutano Mkuu Mchungaji Peter Msigwa kurudi CHADEMA 23/03/2025.
Kashajitenga na CCM.
Je, Urafiki wake na Tundu Lissu Mwenyekiti wa CHADEMA ndo unamfanya alambe matapishi yake?
Mwingine anayepokelewa CHADEMA ni Dr. Slaa.
Kama ikiwa hivyo, CHADEMA itakuwa imezaliwa mara ya pili. Kila la heri
Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM baada ya kutimka kutoka CHADEMA Siku ya Jumapili, Juni 30, 2024, mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho (NEC), katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan. Kama atarudi CHADEMA, atakuwa hajaa huko hata mwaka mmoja.
Mchungaji Peter Simon Msigwa
Msigwa aliikimbia CHADEMA baada ya kushindwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa tofauti ya kura mbili tu, katika uchaguzi wa ndani wa CHADEMA uliofanyika Mei 29, 2024 huku akimshtumu aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, kwa kutumia mamlaka yake kuingilia mchakato wa demokrasia ndani ya chama kulazimisha watu anaowataka yeye ndo wawe washindi.