Anaandika Wakili Msomi Peter Kibatala
Kanuni za Uchaguzi TLS zinaruhusu Mgombea kuchaguliwa/kupigiwa kura hata kama hayupo ukumbini wakati wa Uchaguzi/kupiga kura.
Kuna precedent pia katika chaguzi katika ngazi za chapters mbalimbali hivi karibuni; ambapo wagombea walipigiwa kura licha ya kutokuwepo ukumbini wakati wa uchaguzi/kupiga kura.
Sisi ni Wanasheria na tuna jukumu la kuzitumia sheria na kanuni zetu za Uchaguzi katika namna itakayosaidia kutatua matatizo kama ya kukamatwa kwa Antipas Tundu Lissu Mughwai anayegombea nafasi ya Rais wa TLS.
Kukamatwa kwake Tundu Lissu hakuzuii yeye kupigiwa kura na kuchaguliwa kuwa Rais wa TLS.
Wanasheria mnaopanga kuja Arusha mje kwa wingi wenu kama mlivyopanga, na tushirikiane kuhakikisha Uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu kama ilivyo ada yetu Wanasheria. Case iliyofunguliwa na Bw. Onesmo Mpinzile vs TLS na AG kuhusiana na Uchaguzi huu imetupwa leo na Panel ya 3Judges .Kama mlivyosikia
VOTE FOR TUNDU LISSU