KERO Pesa za refund chuo cha DUCE ni kizungumkuti

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Chuo Cha Duce ( Dar es salaam University College of Education)

Department ya fedha inawasumbua wanafunzi wanaodai refund.

Refund hyo ni pesa ambazo wanafunzi wanapaswa kurudishiwa baada ya wao kulipa pesa kama ada ya masomo nk. Kwa chuo na hali ya kuwa serikali imeidhinisha walipiwe kama mkopo. Hivyo pesa hizo zinapaswa kulipwa kwa wanafunzi stahiki.

Wanafunzi wanaodai refund Toka mwaka Jana mwezi wa saba hadi leo bado hakuna muelekeo wowote kuhusu kulipwa kwa fedha hizo kwani wahusika wanaotaka majibu ya ajiabu, serikali ya wanafunzi Daruso imeshindwa kabisa kwani wakiulizwa hawana majibu na hivyo kutoa ahadi za uongo. Rais wa Daruso, hapokei simu za watu wanaodai.

Kitengo cha fedha Kila wakipigiwa simu wanadai kuwa account zilikosewa tumeanza upya maana fedha zinarudishwa. Nashangaa kusikia hivyo wakati account yangu hiyo hiyo ndiyo napokea na kuweka pesa zangu nyingine.

Walidai mwezi wa tano watu wote watalipwa lakini hakuna kilichotokea. Sasa hivi kila nikimpigia ananiuliza Mimi ni nani wakati awali alikuwa ananifahamy hadi sura.

Mwanzoni kwa mwezi June amepigiwa simu anasema watu wameshalipwa fedha zao kasoro mimi, hivyo niangalie account yangu kama imepokea. Hali yakuwa sipokea chochote ikabid niende CRDB Tena. Nilivyompigia akasema nimpigie wiki inayofuata lakini hakuna chochote.

Wiki ya pili ya June 2024, nilimpigia anasema yeye hayupo ofisini nimpigie wiki inayofuata baada ya wiki ijayo , maana yake itakuwa mwezi wa saba.

Hivi kweli mwaka mzima nafuatilia fedha yangu kwa namna hii.

Mimi nipo mjini na taarifa zangu ninazo zote na nimemaliza chuo 2023.

Je, wale ambao hawapo mjini na hawana mawasiliano nao?

Hili lifikishwe!

Majibu ya DUCE ~ Madai ya Refund ya Wanafunzi Chuo cha DUCE, Uongozi wasema umeshalipa waliosalia ni Wanafunzi 11
 
Nakumbuka mwaka wetu tulipewa on date tena ilikuwa cash sio Kwa akaunti.
Watakuwa wamekula hao
 
Back
Top Bottom