Watanzania bana, cjui tunatakaje. Mawakala wana faida tofauti na mnavyofikiria mawakala wanaongeza efficiency ya ukusanyaji wa mapato pia ni namna nyingine ya kuishirikisha sekta binafsi. Imagine sehemu uliyokuwa ukusanye sh 1000 ukaingia mkataba na wakala wa kukupa 800, manake wakala ataajili vijana vijana watalipa kodi, bima za afya nk pia watasaidia familia zao huko hivyo kupunguza umaskin kwa njia moja au nyingine kwa ile margin ya sh 200.
Ukisema ukusanye ww mwenyew kwanza huwezi kuleta hiyo 1000 yote sababu utaongeza manpower ambao ni waserekali ambao usimamiz wao ni mdogo hivyo pengine kujikuta unalipa watu mishahara wasiofanya kazi na mambo mengi tunayoyajua cku zote na kuyajadili humu.
Me nadhani ambacho ungesema ni kuhakikisha tenda za ukusanyaji zinakidhi vigezo wanapewa wenye sifa, na wanapewa malengo ambayo yataisaidia halmashauri kuraise hela nyingi na kuwaachia margin kidogo mawakala waendeshe ofisi.
Hivi fikirieni wale watu wa parking unadhani jiji lingeweza kuajili watu wote wale, lakin wasingekuwepo unadhani ni vijana wangapi wangekuwa hawana kaxi ya kufanya?
Hii nchi ni masikin ni lazima mipango yote tunayopanga ireflect umaskin wa watu wetu, me nadhan tungeongeza condition za mikataba ya ajira kwa wafanyakaz wa mawakala wakat wa kutoa tenda.