Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 1,124
- 2,194
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu limemfikisha mahakamani Pendo Paul Elikana, mkazi wa Mbuga ya Baya, Wilaya ya Meatu, kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii kuwa amepewa kazi ya kutekeleza mauaji ya kiongozi wa kisiasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Edith Swebe, imesema uchunguzi umebaini kuwa taarifa alizozitoa binti huyo hazikuwa za kweli, bali alizitunga kwa maslahi binafsi na kwa nia ya kupotosha umma.
"Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi, kuepuka kutoa taarifa zisizo sahihi au kuchafuana, ili kuepusha taharuki katika jamii," amesema ACP Swebe.
Soma Pia: Video: Askari akiri kupewa ofa ya kumshambulia na kumwangamiza Luhaga Mpina kwa silaha. Asema maisha yake yako hatarini
Ikumbukwe kuwa mnamo Machi 19, 2025, Pendo alidai kupitia mitandao ya kijamii kuwa alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Mussa Mbuga, aliyemweleza kuwa anataka kumpa kazi ya kumuua Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mhe. Luhaga Mpina