Pendekezo: Mashabiki wa mpira tususie kuingia viwanjani maana hawa TFF, Yanga na Simba wanachezea akili na maisha yetu

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
11,626
41,095
Bila kumumunya maneno, hawa TFF wakishirikiana na hivi vilabu vya Simba na Yanga wamegundua sisi mashabiki wa Soka wa Tanzania ni wajinga, wapuuzi, wapumbavu na wafu. Wanaweza kutengeneza kanuni wanazozitaka wao, wakazistafsiri wanavyotaka, wakatengeneza matukio na kutuyumbisha wanavyotaka wao.

Sasa dawa ni moja, viwanjani hakuna kwenda tena, maana tumegundua Soka la Tanzania ni mchezo wa wahuni wa TFF wakishirikiana na hawa viongozi wa vilabu vya Yanga na Simba kwa gharama ya pesa zetu na kuhatarisha maisha yetu.
 
Mtoa post pole ila huu ni mtazamo wako tu hata mechi ya dabi ikiahirishwa mara ngapi wenye mahaba watakwenda tu
 
Hata bila kususia ni kwamba TFF na ndugu zake wanapunguza washabiki wa mpira bila kujua..
 
Hakika kushabikia sana simba na Yanga kunasababisha kichwani kuwe kweupe.

Fyuzi zinaanza kukata
 
Wazo Zuri Sana kwa sababu shabiki wa mpira wa miguu ndo uti wa mgongo wa mpira wa miguu
 
Bila kumumunya maneno, hawa TFF wakishirikiana na hivi vilabu vya Simba na Yanga wamegundua sisi mashabiki wa Soka wa Tanzania ni wajinga, wapuuzi, wapumbavu na wafu. Wanaweza kutengeneza kanuni wanazozitaka wao, wakazistafsiri wanavyotaka, wakatengeneza matukio na kutuyumbisha wanavyotaka wao.

Sasa dawa ni moja, viwanjani hakuna kwenda tena, maana tumegundua Soka la Tanzania ni mchezo wa wahuni wa TFF wakishirikiana na hawa viongozi wa vilabu vya Yanga na Simba kwa gharama ya pesa zetu na kuhatarisha maisha yetu.
katiba mpya na maisha yako kuhusu uhuru haaaa.ila mpira ndio unaona kijambio chako kimepata uwelewa sana kutafakari
 
Shida ni upangaji matokeo na uhuni wa watu hasa viongozi na wanasiasa kuingilia soka
 
Hii game ilikua haina manufaa yoyote ya kusaidia mbio za October 2025 mlitegemea nini, lazima ihairishwe mambo mengine yaendelee tujipange kwaajili ya mapambio
 
Back
Top Bottom