Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 126,736
- 241,841
Hii ni kwa sababu Bunge aliloliongoza wakati wa awamu ya 5 lilikubali kutumika kuvunja Katiba ya Nchi, jambo liloleta taharuki na Manung'uniko.
Kwa mfano, Kitendo cha Spika Ndugai kuruhusu wabunge waliotimuliwa kihalali kutokana na kusaliti vyama vyao, wakiwemo na wale waliojivua wenyewe ubunge na uanachama, akiwemo Mtakatifu Cecil Mwambe, kuendelea na vikao vya bunge ulikuwa ni uvunjifu mkubwa wa Katiba ya nchi uliotokana na Kiburi cha kulindwa.
Katiba ya Tanzania inawataka wabunge kuwa wanachama wa vyama vya siasa, wakikosa sifa za uanachama wanaondolewa bungeni, hivi ndivyo Ndugai alivyomfanyia Sophia Simba aliyevuliwa uanachama kibabe tu na Magufuli.
Job Ndugai ameshiriki uchafu mwingi uliosababisha bunge letu kudharaulika kupita kiasi baada ya kuokota Kanuni nyumbani kwake na kuamua kuzileta bungeni, akamvua ubunge Mgonjwa Lissu na kuamua kuzuia mafao yake ya halali ili AFE NJAA, hata hivyo Lissu angali mzima hadi leo, Mifano ya uchafu wa Ndugai ni mingi mno na wala hatutaweza kupata karatasi za kutosha kuandika, huyu mtu hafai kuongoza chochote, achilia mbali bunge.
Kwa vile sasa tumeamua kuanza ukurasa mpya, basi ni vema wale wote waliovunja Sheria za nchi kwa manufaa yao, akiwemo Job Ndugai waondolewe Madarakani ili kuliponya Taifa