PAZIA LA FILAMU 🎬📽 : THE HOUSE OF GUCCI

Oct 4, 2023
64
67
FB_IMG_1745313395218.jpg
HOUSE OF GUCCI

Ni mwaka 1978 katika jiji la Milan nchini Italia, nchi ya fasheni na mitindo mbalimbali ya mavazi.

Palikuwepo familia kubwa,
Familia ya Gucci.
Ilikuwa familia tajiri,yenye nguvu na mamlaka kibiashara .Kila kiumbe hai kilichobahatika kuzaliwa kwenye familia hii, kiliishi kwenye pepo ndogo ya utajiri miaka hiyo ya 70. Walimiliki kampuni kubwa ya mitindo ya mavazi,GUCCI.
Ikiwa ni biashara hai, biashara yenye faida...biashara ya kampuni ya familia.

Kwa vile uzee hauna dawa! Na unapopiga hodi kwa mtu...husababisha uchovu wa akili na mwili. Basi uzee ukamfikia Rodolfo Gucci. Asingeweza kuendelea kuuchosha mwili na akili yake katika biashara,
Akaamua kumrithisha mwanae mali zake zote, ikiwemo sehemu ya kampuni ya familia, aendeleze pale alipoishia yeye.

Maurizio mwana wa Rodolfo, alikuwa kijana mtanashati aliyebarikiwa upole na ustaarabu. Maisha yake yalibadilika baada ya kuikaribisha nuru mpya machoni mwake pale alipokutana na binti mrembo-Patrizia Reggiani.
Wawili hawa wakaanza kusafiri pamoja katika bahari ya hisia nzito za kimapenzi. Penzi likamnogea kijana Maurizio, akatangaza ndoa!

Ndoa hii haikubarikiwa na baba yake, baba alimuonya mwanae kuwa huyu binti hana mapenzi ya kweli.
Mzee alimuona Patrizia kama mchimba madini aliyekuja kuchimba dhahabu katika mgodi wa Gucci na kuondoka. Hakumuamini!
"Huyu hana mapenzi ya kweli na wewe mwanangu. Amezipenda fedha zako tu!", alimwonya mwanae.

Lakini sikio la kufa haliwezi kusikia dawa! Maurizio Gucci alikuwa ameshazama kwenye bahari ya mapenzi. Alimpenda Patrizia, akafunga naye pingu za maisha. Akamkaribisha kwenye familia ya Gucci.

Naam! Patrizia binti Reggiani akawa mke wa ndoa wa bwana Maurizio. Na Mungu akalibariki tumbo la uzazi la Patrizia, akawajalia mtoto mmoja wa kike. Furaha ikaongezeka katika ndoa yao.

Patrizia akaanza kujibidiisha sana ili awapendeze wakwe. Na kweli akafaulu, wakampokea kwa mikono miwili mpaka kwenye biashara ya familia. Wakampa kipaza, na yeye akapata sauti kwenye biashara ya kampuni ya familia.
Makosa!!

Baada ya kifo cha baba wa Maurizio, mzee Rodolfo; Yule Patrizia mchimba madini haramu aliyetabiriwa akaanza kuonekana. Patrizia alikuwa ameonja asali ya heshima ya damu ya Gucci, akataka kuchonga mzinga kabisa.
Shetani wa ubinafsi na ulafi akampitia, akataka apande matawi ya juu kabisa kwenye biashara hii ya familia.
Akadai heshima na mamlaka sawa na ndugu wa damu ya Gucci. Tamaa!!

Muda huu wote, Maurizio alikuwa kipofu wa mapenzi. Akawa kama Ngoswe!
Mapenzi yake na uaminifu kwa mkewe, vikamsahaulisha majukumu na wajibu wake wa kibiashara. Akampatia usukani mkewe aendeshe biashara!
Patrizia akataka gari zima.

Likapikwa bomu ndani ya ndugu wa familia moja ilikuwaangamiza ndugu mmoja baada ya mwingine.
Bomu la fitina, usaliti na chuki!
Familia ya Gucci ikasambaratika.
Maurizio anashtukia kuwa ameuharibu umoja wa damu ya familia yake kupitia mikono yake yeye mwenyewe.
Tena kwa mipango miovu ya mke wake, mke ambaye sio wa mzaliwa wa damu ya familia ya Gucci.

Lakini alikuwa amechelewa sana. Sawa na kukumbuka kujifunika shuka saa kumi na mbili asubuhi.
Kupitia ndoa yake, anaharibu kila kitu.

Kampuni inaponyoka kutoka kwenye umiliki wa familia ya Gucci mpaka kwa watu wa nje ya familia. Damu inazidiwa uzito na maji!
Ni filamu nzuri sana kuitazama, ina elimu ya kutosha na burudani pia. Inaitwa HOUSE OF GUCCI imetoka mwaka 2021. Kaitazame.

Godlove Kabati,
22. April 2025,
Morogoro, Tanzania.
 
Nimej
View attachment 3311922HOUSE OF GUCCI

Ahsante sana
 
Back
Top Bottom