Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 25,436
- 18,879
Ndugu zangu Watanzania,
Kwa hakika hakuna chama cha upinzani kwa sasa wala kiongozi wala mtu yeyote yule kutoka upinzani ,anayeweza kufanya mkutano mkubwa ambao ukahudhuriwa na maelfu ya wananchi kama Mheshimiwa Paul Makonda Jabali na Nguli siasa na kijana jasiri kuwahi kutokea kusini mwa jangwa la sahara.
Mheshimiwa Paul Makonda alipotua na kukanyaga mkoa wa Mbeya na kufanya mkutanoni wa hadhara ndani ya ardhi ya mkoa wa Mbeya alipokelewa na umati wa maelfu ya watu waliofurika na kumiminika kama mchanga wa baharini. ilikuwa hakuna pa kukanyaga wala kusogeza mguu.ilikuwa ukitoa mguu wako basi utaishia kukanyaga juu ya mguu mwingine wa mtu ,maana hata sisiminzi asingeweza kupata nafasi ya kupenya kwa namna watu walivyokuwa wamefurika na kujaa utafikiri enzi zile za marehemu askofu dkt Moses kulola alivyokuwa anapokelewa huku kwetu.
Mikutano yote ya Mheshimiwa Makonda imekuwa hivyo hivyo ikipata mapokezi makubwa kwote anakopita na kufanya mikutano.watu wamekuwa wakijitokeza kwa wingi sana,.jambo ambalo limemtisha na kumtetemesha sana Mbowe mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ambaye akiwa mkoani Mwanza alianza kulia lia kuwa mafuriko ya Mheshimiwa Makonda ni ya kutengenezwa kwa kuwalazimsha watu kuhudhuria, lakini cha ajabu ni kuwa yeye mbowe ameshindwa kuyatengeneza na kuwalazimsha watu..
Sasa jana ndipo ikaonyesha ukubwa,uzito na thamani ya Mheshimiwa Makonda katika mioyo ya watanzania hasa wanambeya ambako mkutano wa hadhara ulifanywa na CHADEMA.kwani licha ya CHADEMA kusombelea watu kutoka mikoa yote ya nyanda za juu kusini lakini bado hali ya mahudhurio yawatu haikufikia hata robo ya mafuriko ya watu waliompokea Mheshimiwa makonda.hii ndio sababu jina la Mheshimiwa Makonda lilitawala katika matembezi yao ya kupoteza muda waliyokuwa wanayafanya CHADEMA.
Nilishuhudia magari hasa macosta yakisombelea watu kutoka mikoa yote ya jirani na wilaya zake yakiwaleta watu Mbeya ili wafanye maandamano jana.lakini hawakuweza kujaa hata kwenye kiganja.ndio maana picha za mitandaoni waliziweka kijanja janja ili kuficha aibu.lakini kwa tulioshuhudia na kuona tulibaki tunawasikitikia tu CHADEMA kwa namna kilivyopoteza ushawishi na nguvu kwa watanzania.kwa sasa watu hawana habari na habari za CHADEMA.ndio maana watu walikuwa wapo Bize tu kuendelea na kazi na shughuli zao.
CHADEMA wakubali tu kuwa hawawezi kushindana na Mheshimiwa Makonda wala CCM, Maana Mheshimiwa Makonda mmoja tu anawatoa jasho na kuwashinda.vipi kikiingia chama kizima na idara zake zote? Mheshimiwa Makonda pekee yake akitia mguu mahali fulani anateka mkoa mzima na kuwa gumzo mitaa yote ,ambapo shuguli zote husimama ili kwenda kumsikiliza. lakini CHADEMA pamoja na makelele yao ya magari kutangaza kila siku lakini watu hawakuwa na habari nao na badala yake waliamua kuendelea na shughuli zao.
Hii ni kwa kuwa wananchi wanatambua kuwa palipo na Mheshimiwa Makonda na CCM yake ndipo mahali unapoweza kupata majibu ya kero yako, ndipo unapoweza kupata suluhu ya shida yako ,ndipo unapoweza kufutwa machozi yako,ndipo unapoweza kusaidiwa na kupewa msaaada wa hali na mali,ndipo unapoweza kusikilizwa bila kujali hali yako na kupewa majibu stahiki.
Sasa ukienda kwenye mkutano wa CHADEMA utaishia kusikia matusi na makelele yasiyo na tija wala majibu ya kero za watu wala msaada kwa mwenye shida. Watu kwa sasa wana imani kubwa na Mh Makonda na CCM yake kwa ujumla na ndio maana kwa sasa wana kiu kubwa sana ya kuona Mh Makonda anarejea jukwaani na kuendelea na ziara zake baada ya kuwa amesitisha kwa muda kwa ajili ya kushiriki mazishi ya hayati Edward lowassa.
Nawaonya CHADEMA kuwa acheni kushindana na Mh Makonda. kumshambulia ni sawa na shambulizi kwa watanzania wanyonge ambao wanamtizama Mh Makonda kama mtetezi wao ,sauti yao na kimbilio lao la Haraka juu ya kero na shida zao katika kupata msaada.kwa hiyo mkijaribu kutaka kushindana naye basi mjue kuwa mnashindana na kupambana na mamilioni ya watanzania wanyonge ambao wapo nyuma ya Mheshimiwa Makonda ,kumuombea dua njema na kumshukuru Mungu kwa kumpa maono Rais wetu kipenzi Rais Samia ili kuwaletea Mheshimiwa Makonda atakaye tembea nchi nzima kuwasikiliza kero zao na kuzifikisha kwake na serikali yake.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.