Paul Makonda, Amos Makala na Joyce Ndalichako wana bahati ya kuteuliwa ila wana uwezo mdogo sana wa mikakati na uongozi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,063
4,840
Kuna watu wamezaliwa na bahati ila capacity na creativity hakuna. Watu kama Makonda wanachoweza nikudhalilisha wengine siyo kufanya kazi. Maisha yao yote wanaamini wao wanapaswa kuongoza na wanapoongoza basi akili zao zinapaswa kuheshimiwa. Makonda amerudishwa ofisin tu anaanza kugombana na wale aliowadhulumu. Hata ukuu wa mkoa alipaswa asipewe maana amethibitisha hawezi kujifunza na akipata madaraka makubwa zaidi lazima ataendelea kuumiza wale anaoamini wanapaswa kumwabudu.

Ndalichako ni mwanataaluma lakini siyo mwanasiasa, analazimika kukaa kwenye ulingo wa siasa kwa sababu anateuliwa na kuongozwa na wanasiasa. Alipaswa kuwa mkurugenzi au katibu mkuu wa wizara akae kama mtaalamu

Amos Makala anabebwa na uzee wake kwenye chama na kukua mikononi mwa wanaotawala. Lakini katika maisha yake hakuna remarcable issue amewahi kufanya.

Hawa watu na wengine wa sampuli hii tungekuwa na mfumo wa usahili wasingepata kazi.
 
Back
Top Bottom