wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 503
- 1,421
Ukose Hela akukatae haupo bize, utafute ela akukatae uko bize
Kocha mkuu wa Manchester City ya Uingereza Pep Guardiola ameachana rasmi na mke wake Cristina Serra baada ya kudumu kwenye ndoa miaka 30. Katika talaka waliyopeana mahakamani mke huyo wa Guardiola atatwaa nusu ya utajiri wa Guardiola na jumba lake kubwa la kifahari lililopo jijini Manchester nchini Uingereza.
Vyanzo vimetathmini utajiri wa Pep kuwa dola za kimarekani milioni 126 sawa na shilingi bilioni 318
Sababu kuu ya mke huyo kuomba talaka ni yeye kudai Guardiola yupo bize na kazi.
Guardiola na mke wake katika miaka 30 ya ndoa wamefanikiwa kupata watoto watatu Marius, Maria na Valentina
Inadaiwa mgao huo umempa stress zinazochangia timu anayoifundisha Manchester City kufanya vibaya msimu huu.