The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 365
- 713
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis, amepewa gari jipya la kisasa aina ya Mercedes Benz linalotumia umeme pekee likiwa ni gari la kwanza la aina yake kutengenezwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya Kiongozi huyo ambapo hatua hiyo inayoonyesha azma ya Vatican kulinda mazingira na kuhimiza matumizi ya teknolojia rafiki kwa dunia.
Hafla ya kukabidhi gari hilo ilifanyika katika Uwanja wa Vatican ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Mercedes-Benz, Ola Källenius, alimkabidhi Papa funguo za gari hilo na kumuelezea muundo wa kipekee wa ndani.
Gari hilo lililotengenezwa kwa msingi wa mfano wa Mercedes-Benz G580, lilichukua mwaka kutengenezwa na limewekewa teknolojia maalum inayoliwezesha kwenda kwa mwendo wa polepole unaofaa kwa hafla rasmi za hadhara ambazo Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki hufanya.
Mercedes-Benz imekuwa ikitengeneza magari maalum kwa ajili ya Mapapa kwa karibu miaka 100 kuanzia mwaka 1930 wakati Papa Pius XI alipopokea gari la kwanza kutoka kampuni hiyo ambapo tangu wakati huo, Mercedes-Benz imeendelea kuboresha magari yake ili kukidhi mahitaji ya viongozi wa kidini kwa umaridadi na teknolojia ya kisasa.
Chanzo: Millard Ayo