The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 832
- 1,423
Baada ya ombi la kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis kwa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kulegeza sera yake dhidi ya wahamiaji haramu kwamba utekelezwaji wake unawakandamiza wahamiaji haramu waliokimbia umasikini na machafuko kwenye mataifa yao, mshauri wa masuala ya uhamiaji wa serikali ya Trump Bw. Tom Homan amemjibu vikali kiongozi huyo wa kanisa na kusema hata kanisa hilo haliruhusu wahamiaji haramu, shirika la habari la Marekani Voice of America limeripoti taarifa hiyo nmekuekea hapo chini kwenye comments
Homan amesema hata Vatican (makao makuu ya kanisa hilo) imejengewa ukuta na ni kosa mtu kuingia ndani ya eneo hilo la kanisa bila kibali na iwapo akiingia na kukamatwa huchukuliwa hatua kali za kisheria kwa kutishia usalama wa eneo hilo
Homan amemsihi kiongozi huyo wa kidini kujikita kufanya marekebisho ya kikanisa ila suala la uhamiaji haramu Marekani amuachie Trump kwakua ni wajibu wake kama Rais kudhibiti wahamiaji haramu na uhalifu
Trump kaweka vyuma tupu nyuma yake aisee...