kajekudya
JF-Expert Member
- Sep 24, 2015
- 2,467
- 4,910
Tanzania ni moja ya Nchi ambayo baada tu ya Uhuru ilifanikiwa kujenga msingi Imara wa kiutawala kupitia TANU na baadae CCM. Msingi ambao unaifanya Tanzania kuwa moja ya Nchi chache Barani Afrika zenye uimara wa hali ya juu kiutawala.
Sasa ni miaka 20 tangu mfumo wa vyama vingi uanze, na hakuna shaka huu ndio mfumo ambao kwa sasa unakubalika Kama mfumo sahihi. Ndani ya miaka hiyo 20 Tanzania tunayo bahati ya kuwa na moja ya vyama bora vya Siasa duniani, CHAMA CHA MAPINDUZI na kupitia Chama hiki tumeendelea kuwa Taifa Madhubuti sana.
Ni bahati Mbaya kuwa ndio Chama pekee chenye mlengo unaoeleweka, Sera zinazoeleweka, Muundo unaoeleweka na kinachoendeshwa kisomi na kwa tafiti. Vyama vingine ni aidha vimejengwa juu ya Migongo ya watu au ni vikundi vya watu wachache ambao wakichuja kisiasa vyama vyao navyo huchuja. Mifano ni Mingi, leo CUF ni Kama imekufa baada ya Maalim Seif kuhamia ACT, CDM hadi leo wanamg'ang'ania Mbowe kwakuwa hawajui hatima yao bila yeye, ACT Kila ukiiangalia unamuona Zitto Zuberi Kabwe, hivyo hivyo kwa NCCR Mageuzi na Mbatia.
Udhaifu huu wa vyama hivi pamoja na kuwa fursa kwa CCM kuendelea kutawala, kwangu naouna kama wenye hatari Sana kwa Mustakabali wa Taifa hili. Lazima tukubaliane si Watanzania wote wanaoukubaliana na Sera za CCM Wala wanaipenda CCM. Mshkaji ninaye kaa naye Mimi haielewi CCM kabisa tarehe 28/10/2020, nilimuamsha asubuhi tukaongozana kwenda kupiga kura, yeye alikwenda kumpigia kura Lissu mimi nikaenda kumpigia kura Magufuli na tuliondoka tukifahamu hilo. Kwenye Group langu la Whataup O level tulikuwa na jamaa mmoja yeye alikuwa amekuwa Kama kichaa kwa Lissu, humwambii chochote, kila sekunde anaposti mpaka Wana group mnakereka. Na Hawa wapo wengi sana.
Ninachotaka kusema watu hawa wanahitaji kupatiwa sehemu ya kupumulia, sehemu hiyo iwe sehemu Madhubuti, inayoeleweka na inayoaminika. Wasiwe watu wa hovyo hovyo au kikundi Cha hovyo hovyo.
CCM pamoja na mambo mengine inaendelea kushinda Uchaguzi kwakuwa inaaminika. Hivo Kama Taifa tunahitaji kupata Chama kingine ambacho kitakuwa Cha Ki taasisi, Chama kinachoendeshwa kiweledi na chenye watu wanaoeleweka na Cha Kizalendo Kama na kiaminike kama kilivyo CCM lakini chenye mlengo tofauti na CCM.
Kuendelea kuwa na vyama dhaifu ndicho kinapelekea kuwa na Wagombea aina ya Lissu, ambao hawajui kwanini wanagombea lakini waliondaliwa ughaibuni na kwakuwa watu wenye mlengo tofauti na CCM hawana sehemu sahihi ya kupeleka machaguo yao wanalazimika kuwafata watu wa aina hiyo.Hivi tumejiuliza inaweza kuwa Inchi ya Namna gani!? Rais Lissu, Makamu Salumu Mwalimu, Mwenyekiti wa Chama Mbowe, Katibu mkuu wa Chama Mnyika, wajumbe wa CC, Halima, Lema, Msigwa, Sugu, Prof Jay, Bulaya na Boniface Jacob.Yes Hawa ndio walikuwa wanatafuta Dora na hakuna shaka kwa kiasi kikubwa walipata uungwaji mkono ni mjinga pekee anaweza kubeza Hilo.Kwa lugha rahisi Hawa ndio walikuwa wanaomba kuliongoza Taifa, Hawa ndio wangekuwa wanatoa maamuzi mazito juu ya Mustakabali wa Taifa.
Sasa ili kuondoa wasiwasi wa kuwa na vyama vinavyojengwa juu ya watu, na kuhatarisha ustawi wa Taifa hasa pale watu watakapoamua kuvichagua baada ya kuichoka CCM, kama Taifa na hasa Kitengo, wafanye uratibu wa kupata Chama kingine Cha Kizalendo na ambacho kitakuwa na mfumo Imara wa kitaasisi na kinachoeleweka ili kiweze kuwa Chama shindani kwa CCM na kiwape Watanzania wasiovutiwa na kukubaliana na Sera za CCM mbadala lakini pia kiwape nafasi Watanzania chaguo pale wanapokuwa wameichoaka CCM, na chaguo Hilo liwe ni Taasisisi inayoaminika na yenye uwezo Kama CCM, ili kuepuka hatari ya kupata mbadala wa aina Lissu ambao kiukweli ni hatari kwa maslahi ya Taifa.
Na kwakuwa sasa tutakuwa na Chama au vyama Mbadala visivyotiliwa shaka, kitaasisi, kimuundo, Kizalendo na kuiuwezo, basi na mfumo mzima wa Uchaguzi ufumuliwe hasa ikiwemo Tume ya Uchaguzi na mfumo mzima wa usajiri wa vyama ili kuondoa minongona na hisia zinazotokana na ground level isiyo na uwiano, na hii itasaidia mtu anaposhindwa akose visingizio na hata akivitoa watu waone havina msingi.
Kwa Sasa hata Chama kingepata kipigo Cha Mbwa Koko Kama walichopata Mwaka huu na ambacho kipo dhahiri na ambacho wengi tulikiona Mapema na kukitarajia bado wakitoa Malalamiko yanaweza yakaonekana yana mantiki. Hadi Uchaguzi unafanyika Rais alikuwa ni Magugufuli na ambaye alikuwa anagombea katika Uchaguzi uliosimamiwa na Tume aliyoichagua yeye, Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya aliowachagua yeye na Majaji aliowaachagua yeye. Hakuna shaka ushindi wa aina yeyote Katika Mazingira haya lazima watu wauhoji. Yaani ni sawa na Simba ya Haji Manara Leo icheze na Buyern Munich na wafungwe Goli 100, lakini Refa wa Kati akiwa ni Mwenyekiti wa Buyern Munich, navibendera wakiwa CEO wa Buyern na Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Ujerumani, Ushindi huo pamoja na tofauti kubwa ya ubora Kati ya timu hizi bado unaweza kuhojiwa.
Kwahiyo sisi Kama Taifa tunayo fursa kwakuwa tayari tunacho Chama kimoja Imara na Madhubuti sana, na ambacho kimefanya tuwe na Taifa Madhubuti. Lakini ukweli unabaki kuwa Watanzania hawawezi kuwa milele wanaichagua CCM, ipo siku wataamua tofauti, hivyo tunao wajibu wa kuhakikisha tunajenga Taasisisi za kisiasa Imara na zinazoaminika ambazo Kama ilivyo CCM zitakuwa na uwezo wa kuliongoza Taifa hili kwa Uzalendo pale Watanzania watakapoamua kuipumuzisha CCM.
Nimevaa ngao