Pamoja na kujulikana mambo yako maovu ila kuna vitu vidogo/mambo madogo madogo ila vinakuongezea thamani yako

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
21,212
50,145
Ushawahi kuona mtu Ana skendo chafu chafu haswa za umalaya uliopitiliza au ulevi na ukorofi lakini ukashangaa anaitwa kuketi katika karamu ya wakubwa na anashirikishwa michongo.?


Kuna watu wamejua sana kucheza na Saikolojia kiasi kwamba hata akisimulia yeye au ukishuhudia starehe zake chafu ila bado hata wewe mwenyewe unamtetemekea fulani sisemi unamuogopa ila title yake unabaki kuiheshimu Balaa..


Sasa fanya yafuatayo ni dondoo ndogo ndogo ila kama kazi yako inahitaji upate wateja ndo upate hela.

1.toa toa tips unapoenda kufanya manunuzi kama unajua siku hiyo uko vizuri kipesa basi sio kila chenji ya kudai nyingine ndogo ndogo ziache kama ni bar au dukani au hotelini..

2.vaa sometimes hata zile culture za kimasai yaani means onyesha unajali bidhaa zilizotengenezwa local support local talents


3.kama una hela unapoenda hotelini au mgahawani onyesha kupendelea kutengenezewa chakula unique. Si pesa inaongea mkuu mfano unaweza kwenda sehemu za chakula ila ukaagiza kitu ambacho hawana ili wakitengeneze uwalipe including posho yao kidogo plus tip.

4.kuwa na vitu fulani unique wasivyomiliki watu mfano watu wengi hawavai coat za jeans zile we ndo piga style ile hasa Kwa vijana au unaweza kuwa na ki simu kidogo labda vile vya Nokia au vile vya ku slide onyesha una vitu fulani hivi na una memory navyo.

5.kwenye mazungumzo na mtu ukigundua ana Nia ya kuwachekesha msaport mfano na wewe cheka jifanye huku sikia vizuri arudie Tena kichekesho chake ili upate nafasi ya kucheka Tena.

6.usiwe na nidhamu ya uwoga sometime zima zima simu hata usiku au usipokee maksudi unless awe ndugu pengine kuna dharura ila marafiki au wafanyakazi wenzako kama sio muda wa kazi vunga wakutafute kesho waambie ulikuwa umepumzika wajuage tu hupokei simu sana.

7.tembea na miguu kama una lengo la kufanya mazoezi kunyosha miguu au upo around kikazi kazi. Sio muda wote unazurura tu na miguu hata kama huna gari vitu vingine agiza.. Waamini hata bodaboda sometime unamuita unamtuma vitu sokoni akufanyie yeye akununulie wewe na pia utakuwa umempa riziki sio Kwa sababu ya uchoyo au ubahili basi unaenda zako kuhemea vitu masokoni huko..Tena ukimtuma boda labda akaleta kitu ambacho sio bora sana mfano kimeharibika jifanye hiko ndo kizuri yaani kaleta Viazi vibovu ila we jifanye hivo ndo huenda vizuri utavila cheka kisha muache aende..
 
Back
Top Bottom