Pamba Jiji wavunja Mkataba na Kocha wao Goran Kopunovic

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
3,136
5,023
Sema tayari kimeumana! Hawa Pamba Jiji Championship inawaita mzunguko wa kwanza tu 😃​
1729093693852.jpg

Uongozi wa Klabu ya Pamba Jiji Fc unautaarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu Goran Kopunovic.

Lakini pia umefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya wasaidizi wake, Salvatory Edward, Kocha wa magolikipa Razack Siwa na kocha Viungo Cirus Kakooza.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Mathias Wandida aliyekuwa kocha wetu wa U-20 hadi hapo atakapotangazwa kocha Mkuu.

Uongozi unawashukuru kwa muda wao wote waliokuwepo hapa klabuni na unawatakia kila la kheri katika maisha yao nje ya Pamba Jiji.

Imetolewa na:
Ezekiel Ntibikeha,
Kaimu C.E.Ο,
16 Oktoba, 2024
 

Amos Makalla umeondoka na Pamba Jiji 😔
 
Mzungu wa watu wamemvunjia mkataba mapema
Huyo mzungu amewahi kufanya maajabu kwenye team gani hapa Tz? Alikaribia kuishusha daraja Tabora Utd, kama si uongozi kufanya maamuzi magumu ya kumtimua dakika za lala salama Tabora ingekua championship muda huu. Kutimuliwa Pamba lilikuwa suala la muda tu kutokana na mwenendo wa team. Huyo na Mwinyi Zahera ni mapacha.
 
Back
Top Bottom