Pakiti ya tambi yapanda maradufu kutoka 1000 mpaka 2000

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,155
Hali ni mbaya sana pakiti ya tambi mwezi wa 11 ilikua shilingi 1000 dukani sasa hivi ni 2000
Hivi mtu mwenye akili timamu atadhubutu kuusifia huu utawala usio na huruma kiasi hiki?

Wafanya biashara wadogo wenye vijiduka vidogo vya mtaji wa laki 2-5 wanakamuliwa kwa kodi kila mwezi na TRA

Mnawaacha wawekezaji wanapewa kuchimba madini miaka 5 bure halafu mnajifagilia unafiki tu hapa

Hakuna mwenye akili timamu atakayeusifu utawala huu

Ebu fikiria unalipa umeme kwa mwezi 10000 kodi ya nyumba 50000 kwa mwezi maji 8000 kingamuzi 15000. nauli chakula hujaweka, matibabu, kodi ya biashara, msaidizi nyumbani 80000

Hivi kweli hii serikali inafahamu haya wanafumbia macho?

Maisha yamekua magumu kwa sababu ya sera za kijuba za awamu hii

Sijuti kumpa yule mzee wa ukawa kura yangu tanzania bila sera mbadala tena isiyo ya ccm ni sawa na bure

Mimi yakiitishwa maandamano ya kupinga hali ya kimaisha nipo tayar
Nishachoka kila siku sitaacha kuwalaani watawala hawa
 
Mkuu uko mkoa gan tambi 2000/=?, cc huku toka June bei yake 1500/= na haijabadilika
 
Mimi najiuliza kama hawa watu wanazijua principles za uchumi,moja ya malengo(infact lengo kuu) la contractionary measures ni ku-curb inflation,..the outcome,pesa wamebana na inflation inaongezeka..somewhere somehow pesa inapigwa kisirisiri.
 
Jumuiya za kimataifa zisaidie tupate tume huru ya uchaguzi Tanzania.
2020 kataa ccm kabisa
 
Ebu fikiria unalipa umeme kwa mwezi 10000 kodi ya nyumba 50000 kwa mwezi maji 8000 kingamuzi 15000. nauli chakula hujaweka, matibabu, kodi ya biashara, msaidizi nyumbani 80000
Loan Board 70000+
Income tax 130000+
NHIF 20000+
PSPF 50000+
Mkopo bank 100000 +

.............. WANANCHI WA TANZANIA TUNAISHI KWA MAAJABU,, WE MAKE OUR OWN RECORDS.
 
Loan Board 70000+
Income tax 130000+
NHIF 20000+
PSPF 50000+
Mkopo bank 100000 +

.............. WANANCHI WA TANZANIA TUNAISHI KWA MAAJABU,, WE MAKE OUR OWN RECORDS.


yaani wanapunguza kipato cha raia huku wanapandisha gharama za maisha.... yaan wanapiga kotekote!

ni wakati wa kuishi kama mashetani
 
Tutanunua tu,kwan lini watanzania kipaumbele chao ni tambi? Turudi wakat uliopita nyie nyie mlikua mnalalamika hali ngumu sasa Leo mnalalamika nn tena,,tutakula tu wala usijali ndugu buku mbili unakuja kabsa mishipa ya shingo inakutoka khaaaa,,,mbona bia zikipanda hatulalamiki?juzi tumeshuhudia uwanja iringa umejaa diamond kapaform watu wanakula bata tu we unalalamikia tambi....khaaa
 
Kura za Lowasa huwa haziibiwi hata moja.

Tunachukua nchi asubuhi. ----In nyumbu's voice
 
Ww unaishi mkoa upi huku kwetu caton ni sh 21000 sawa na 1050
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…