Pacha wangu

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
22,326
41,013
Wangaluka wosee,

Leo nimekumbuka pacha wangu, tulizaliwa pamoja, kwa maana ya kwamba tulikaa ndani ya tumbo la mama kwa miezi 9. Haikuwa mipango ya Mungu pacha wangu tulitengwa nawe nikiwa na miaka 12. Nakukumbuka ulivyokuwa mrembo sana pia alikuwa machachari kama Kasie, natumai bado umeutunza urembo wako wa kisomali. Leo tangu asubuhi taswira yake imenijia kichwani..... na haitaki kutoka.

Huko uliko pacha wangu Kalunde jua ya kuwa Kasie mie nakupenda, japo hatujaonana wala kusikia sauti ya kila mmoja tangu tukiwa na miaka 12 ila sauti yako bado naisikia ikiniita. ... Kasie kimbia baba anakuja na fimbo utachapwa. .......

Hakika nimekukumbuka, nakupenda Kalunde pacha wangu. Huko uliko natumai unaendelea vema na maisha.

Siwezi sema zaidi pacha. ...... nimekukumbuka mnoo.

Kasie na Kalunde.
 
Haya tenaaa MTOTO wa Kisomali anatangaza deal,safi kishua na mwenye hitaji arushe shilingi NDI NDI NDI.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…