Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,498
- 7,056
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar.
Othman amechukua fomu hiyo leo Aprili 13,2025 majira ya saa 4.00 asubuhi ikiwa ni mwanachama wa kwanza kwa nafasi ya urais kuchukua fomu hiyo akikabidhiwa fomu hiyo na Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya ACT Wazalendo, Mhene Said Rashid.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Othman amesema "Leo sio siku ya kuzungumza ,nitakuja kuzungumza siku ambayo nitarejesha fomu April 16 mwaka huu"alisema Othman.
Chama hicho ni miongoni mwa nyama 18 vilivyosaini kanuni za maadili ya uchaguzi 2024 ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari Kiongozi wa Chama hicho Ndugu Semu Dorothy alikwishatangaza nia ya kuwania nafasi hiyo.