real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,296
Mashabiki wengi wa soka hupenda kujua mishahara ya wachezaja mbalimbali, lakini kwa upande wa Tanzania, mishahara hii huwa ni siri sana. Si mishahara tu, hata ada za uhamisho kwa wachezaji hawa huwa haziwekwi hadharani kama inavyokuwa kwa wanaocheza soka barani Ulaya.
Taarifa ambazo hazijathibitisha na klabu ya Simba zimesambaa mitandaoni zikionyesha majina ya wachezaji wa Simba pamoja na mishahara wanayolipwa.
Katika orodha hiyo, Haruna Niyonzima aliyesajiliwa msimu huu akitokea Yanga analipwa Tsh milioni 8.7 huku Emmanuel Okwi naye aliyerejea klabuni hapo akishikilia nafasi ya pili kwa mshahara wa Tsh 7.6 na John Bocco liyetokea Azam akilipwa Tsh 6.9 milioni.
Chanzo: Swahili Times