Orodha ya matukio ya majambazi kuua polisi hii hapa.Ni uhasama, siasa au umaskini?

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Salam wakuu na poleni sana na mauaji ya askari wetu Wilayani Mkuranga ,Pwani.


Hapa nchini Tanzania na hasa Mkuranga na Kibiti Mkoani Pwani kumekuwepo na matukio ya majambazi kuua polisi aidha kwa makusudi, kwa uhasama, kulipiziana visasi au kwa sababu ya ugumu wa maisha.


Jambazi aua polisi na kujeruhi 4 kwa bomu - October 8, 2016


Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda ,49, Mkazi wa kijiji cha Uvinza.Mtui amewataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.Amesema askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza Madukani alikokwenda kununua mahitaji.Ameongeza kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa asiuawe kwa kipigo.“Mtuhumiwa alipohojiwa alisema alificha bunduki kijijini kwao Lukole Wilayani Ngara Mkoani Kagera, ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa ardhini,” amesema Kamanda Mtui.Aidha, walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne (risasi 30 kila moja) na mbili (risasi 20 kila moja) na risasi 75 zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa.Hatahivyo, askari huyo alifariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni) huku majeruhi wote watano wakipata matibabu hospitalini hapo na kuruhusiwa kurudi nyumbani.


Arusha yarindima kwa risasi! Jambazi laua polisi -Nov 11, 2011


KATIKA hali isioyokuwa ya kawaida askari polisi F 228 Constebo Kijanda Mwandru amefariki dunia, pamoja na mkuu wa upelezi wilaya Faustine Mwafele kujeruliwa vibaya na jambazi sugu mkoani hapa ambaye amejulikana kwa jina la Hendry Samson Kaunda. Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Andengenye Thobias alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saakumi za alfajiri.


JAMBAZI AUA MMOJA NA KUJERUHI MMOJA SERENGETI - January 18, 2013

MTU mmoja amekufa na mwingine kujeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi na kuporwa simu na tsh,40,000= mtu anayedhaniwa jambazi katika kijiji cha Nyamirama kata ya Rung’abure wilayani Serengeti wakitoka kustarehe.


Tukio hilo limethibitishwa na polisi wilayani hapa na ofisa mtendaji wa kata hiyo linadaiwa kutokea januari 17,majira ya saa 4:00 usiku mwaka huu katika kijiji hicho.


Jambazi Awajeruhi Kwa Bomu Askari na Raia Wanne Kigoma - October 18, 2016

Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14.

Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji hicho. Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.
Alisema askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza Madukani alikokwenda kununua mahitaji.
Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa asiuawe kwa kipigo.

Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera, ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa ardhini.



Mkuranga, Pwani: Majambazi yaua Askari Polisi SABA

Jamani habari za usiku. Sisi huku BUNGU eneo la JARIBU mpakani tumepotelewa na askari saba(07) wa kikosi cha FFU.


Ilikuwa hivi:

Askari walikuwa wana-liviana ambapo section moja ilikuwa inatoka na nyingine inaingia. Sasa wakati hii inayotoka baada km 03, Jambazi/Gaidi lilikuwa limejificha porini karibu HIGHWAY baada ya gari kulikaribia jambazi/gaidi hili lilimshambulia dereva kwa mbele na gari kupoteza mwelekeo na kuanguka wakati huo jamba/gaidi liliendelea kushambulia.


Jambazi/gaidi alikuwa mmoja


MASWALI YAKUJIULIZA:

1. Ni uhasama?

2. Ni ugumu wa maisha?

3. Ni kulipiza visasi?

4. Ni ulimbukeni?

5. Ni sifa?
 
Juzi kati tuu polisi walijitapa kuwauwa watu waliodhaniwa ni majambazi daraja la mkapa kwa kudai walishindwa kusimama baada ya kusimishwa wakiwa na bodaboda. Cha ajabu taarifa hizi hazijawahi kuthibitisha walio uawa km walikuwa majambazi au la!

Kuna wakati pia nilisikia kuwa wale watu Saba mto ruvu walikuwa watoto wa mzee fulani huko sijui kibiti waliouawa na walinzi wa Mali asili habari hizi pia zilipuuzwa.

Ukiangalia kwa umakini utagundua kuna kulipa kisasi kwa serikali na vyombo vyake vya ulinzi. Waziri wa mambo ya ndani ukimya wako si wakiutendaji, chukua hatua kuchunguza ku nani? Sababu hasa ya mauaji, kosa kubwa mnaonekana kuwasaka wauwaji badala ya kuchunguza sababu pia ya mauaji hii inaonesha kuna kitu hakiko sawa.
 
QUEST TO ASK KWANINI ?,BAADA YA MAUAJI WANAPORA SILAHA?,TISS KUWENI MAKINI BANA ACHANENI NA MAMBO HAYA...!,
•KWA MAWAZO YANGU,KITENDO CHA HAYA MAJAMBAWAZI KUPORA SILAHA KINAASHIRIA KUNA KITU AU JAMBO WANA-FORM AU WANAANZISHA THATS WHY WANACOLLECTS LOT OF GUN KIDOGOKIDOGO....!,
•NAIOMBA SEREKALI IWE MAKINI KWA HILI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…