Duniani tunaamini kuna mambo mengi sana ambayo bado mwanadamu hajayafahamu, Na hata yaliowahi kufahamika kwa baadhi ya wanadamu kumekua na ugumu kwa watu kuyafahamu,
Basi leo nimekuandikia mambo kumi na tano nikiamini hukuwahi kuyajua..
1. Moto huwaka kwa kasi sana kuelekea juu kuliko kuelekea chini ( kushuka chini ).
2. Kila siku duniani watu zaidi ya milioni tisa huzariwa, Kwa hiyo ukisherekea siku yako ya kuzaliwa , ujue unasherekea na watu zaidi ya milioni tisa.
3. Kwa wastani wa binadamu wa kawaida , ukijumlisha masaa anayolala ni sawa na miaka 25.
4. Mswaki ni kitu pekee ambaacho wasafiri wengi husahau wakiwa wanasafiri.
5. India ndio nchi yenye ofisi za posta nyingi kuliko nchi nyingine yoyote duniani , ( ina ofisi 100,000 )
6. Kwa wastani binadamu wa kawaida anapumua mara 23,000 kwa siku.
7. Urefu wa mguu wako ni sawa na urefu wa mkono wako
8. Kuna kuku wengi duniani kuliko Binadamu, kiasi kwamba kila binadamu ana kuku wake wawili.
9. Binadamu wa kawaida anacheka mara kumi kwa siku.
10. Kwa wastani binadamu wa kawaida atatumia tani 100 za chakula na kunywa maji lita
45,424 za maji kwa mda wake wote wa maisha.
11. Moyo wa mwanamke unadunda kwa haraka kuzidi moyo wa mwanamme.
12. Wanaume hubadilisha mawazo yao mara 2 mpaka 3 zaidi ya wanawake, Wanawake huchukua mda kufanya maamuzi na wakifanya , husimamia maamuzi yao.
13. Raia wa japan hawana majina ya katikati. ( middle names )
14. Huwezi kutoa machoni wakati unamenya kitunguu, kama ukiwa unatafuna jojo ( BIG G )
15. Binadamu atakufa kwa haraka zaidi akikosa usingizi kuliko kukosa chakula, Atakufa ndani ya siku kumi tu.